PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Tamasha la utalii na amani kufanyika Arusha NOVEMBER 22
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mussa Juma,Mwananchi Arusha, Tamasha la Utalii na amani, Arusha tourism Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 22 katika jiji la ...

Mussa Juma,Mwananchi
Arusha, Tamasha la Utalii na amani, Arusha tourism Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 22 katika jiji la Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Golden Rose hotel , Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alisema, tamasha hilo limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media na Alfredo Shahanga Sports  Promotion.
Alisema katika tamasha  hilo, kutakuwa na michezo michezo mbali mbali, ikiwepo soka, mashindano ya riadha ya Tourism Marathon, maonesho ya utalii na kongamano la utalii na amani.
"kauli mbiu ya tamasha hili ni Utalii wa ndani na amani sasa tunatoa wito kwa wadau mbali mbali kujitokeza kushiriki"alisema

Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi Alfredo Shahanga alisema, maandalizi yote muhimu yamekamilika.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wadhamini zaidi kujitokeza  kudhamini ili kuhakikisha wakazi wa Arusha wanashiriki kuhamasisha utalii wa ndani na kuhubiri amani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top