Ndg Patrick Lalika, akiuliza Swali kuhusu Mazingira hatarishi kwa Watoto katika mdahalo
uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao
ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na
Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea
wa Ubunge
|
Mwalimu Nico Mgala, Akiuliza swali kuhusu mrundikano wa wanafunzi madarasani katika .mdahalo
uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao
ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na
Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea
wa Ubunge
|
Ndg Castory Boniface Masangula Mgombea Udiwani kata ya Igowole kupitia CCM akijibu Swali katika mdahalo
uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao
ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na
Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea
wa Ubung
|
Ndg Israel Mpina Msalilwa, mgombea Udiwani kata ya Igowole kwa tiketi ya CHADEMA akijibu swali katika mdahalo
uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao
ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na
Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea
wa Ubunge
|
Wazazi wakifuatilia mdahalo
uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao
ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na
Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea
wa Ubunge
|
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kwenye mdahalo
|
Frank Timothy Malata, mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kusini. Kwa tikeki ya Chadema akitoa maelezo.
|
Mwanafunzi Mangula akiuliza swali juu ya huduma bora ya Umeme
|
Thabiti Msofe Afisa Ustawi wa Jamii Mufindi, Akichangia mada kuhusu Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Lishe Bora katika mdahalo
uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole wilayani Mufindi, ambao
ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi Igowole, Ibatu na
Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao waliwahoji wagombea
wa Ubunge
|
Zikiwa
zimebaki siku 23 kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba
25, hapo jana wakazi wa Jimbo la Mufindi kusini wamewataka wagombea
Ubunge na Madiwani watakaopata nafasi ya kuwaongoza katika kipindi
kinachofuata kutafuta suluhisho la ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni
pamoja na adhabu kupita kiasi kutoka kwa walimu na wazazi, Mimba za
utotoni na kukatishwa masomo kwa watoto kwa ajili ya ndoa ama ajira.
Hayo
yalisemwa katika mdahalo uliofanyika katika Shule ya Msingi Igowole
wilayani Mufindi, ambao ulishirikisha wanafunzi kutoka Shule za Msingi
Igowole, Ibatu na Kisalasi, pamoja na walimu, wazazi na walezi ambao
waliwahoji wagombea wa Ubunge Frank Timothy Malata (CHADEMA) pamoja na
wagombea udiwani Castory Boniface Masangula (CCM) na Israel Mpina
Msalilwa (CCM).
Aidha
walisisitiza suala la upatikanaji wa viwanja vya michezo kwa watoto na
kudai kuwa michezo ni njia mojawapo ya kumbadili mtoto kimwili na
kiakili.
Akijibu
hoja kutoka kwa wananchi, Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo kwa tiketi
ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Frank Timothy Malata
ameahidi kupatikana suluhisho la adha hizo na kukomesha ukatili dhidi ya
watoto. Mgombea huyo pia ameahidi kuinua michezo kwa kuanza na
upatikanaji wa viwanja bora vya michezo mbalimbali zaidi ya mpira wa
miguu.
Kwa
upande wake Mgombea Udiwani Kata ya Igowole kupitia tiketi ya Chama cha
Mapinduzi CCM Castory Boniface Masangula ameahidi kutoa ushirikiano wa
hali na mali kwa kamati za ulinzi za watoto na sekta nyingine
zinazojihusisha na ulinzi wa mtoto ili kuhakikisha watoto wanalindwa
dhidi ya ukatili wowote.
Naye
Israel Mpina Msalilwa ambae ni mgombea Udiwani wa kata hiyo kupitia
CHADEMA aliahidi kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali
kuondoa tatizo la mrundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na kupiga
vita ukatili dhidi ya watoto zikiwemo adhabu kupita kiasi zinazotolewa
na wazazi, walezi ama walimu.
Katika
hatua nyingine, watoto ambao ndio walengwa wakuu wa Midahalo hii
walitoa maoni yao kuwa nini kifanyike baada ya viongozi hao kushika
nyadhifa wanazogombea ambapo walitaja kuwa wanakerwa na uhaba wa vitabu,
vyoo, huduma bora za afya, umeme na usafiri na kupambana na mimba za
utotoni hasa hasa kwa wanafunzi.
Wakati
huo huo, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mufindi Navoneiwa Mfinanga
amewataka wagombea hao kuwa karibu na kamati za watoto ili kuhakikisha
wagombea wanatimiza ahadi zao
Midahalo
hii ni muendelezo wa midahalo ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto
kinachoandaliwa na Kampuni ya TRUE VISION Production chini ya Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ikishirikiana na UNICEF yenye lengo
la kuibua ajenda ya watoto kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Unaweza
kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio
shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi
kuanzia saa tisa mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org nawww .facebook.com/WalindeWatoto
“Tuwape nafasi viongozi wanaojali watoto kwa kutetea haki zao” – Baraza la Watoto
Post a Comment