Watu watano wamefariki dunia papo hapo kwa kukatwa katwa mapanga na kuchinjwa kama wanyama katika kitongoji cha Kisesa kata ya Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
Watu hao ambao ni wa familia moja walifanyiwa unyama huo kwa kukatwa katwa mapanga sehemu ya shingoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa Gemine Mushy
alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9 ambapo Baba, Mama
pamoja na watoto wao 3 waliuawa.
Mushy
aliwataja waliofanyiwa unyama huo kuwa George Charles (30) ambaye ni
Baba wa familia, Siku John (23) Mama wa Familia na watoto wao ambao ni
Mchambi George (7) Tuma George (5) pamoja na Amos George (Miezi 9) wote
wasukuma wa kitongoji hicho.
Kamanda
Mushy alieleza chanzo kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu
(George) pamoja na Baba yake wa kambo ambaye alinunua kipande cha ardhi
alikokuwa akiishi marehemu.
Aliongeza
kuwa baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya msako na kuwakamata
watuhumiwa 3 ambao aliwataja kuwa ni Migata Lusalago (50) Jihelya Migata
(30), Solo Kengele (31) wote wasukuma wa kijiji cha Bugalama.
Kamanda
mushy alieleza kuwa waliokamatwa ni Baba wa kambo wa Marehemu pamoja na
watoto wake wawili ambao ilidaiwa kuwa wameweza kushiriki katika
kutenda tukio hilo la kinyama.
Katika hatua nyingine Mushy alisema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika ili kuwapata wahusika zaidi wa tukio hilo.
Post a Comment