Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la
msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi
wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.
Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili
ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda .
Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania,
Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa
Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).
Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya
Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya
Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.
“Pamoja na bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa
miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na
mitandao ya mawasiliano,” alisema Dk Turuka.
Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha
usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao
wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.
Kwa mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano
wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika
kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza
ajira nchini.
Kuanzishwa kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008, Rais Jakaya Kikwete
alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na
kuafikiana kujenga bandari hiyo.
Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa
Post a Comment