NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu
ya JKT Oljoro mwishoni mwa wiki ilitembeza kichapo kutoka kwa timu ya Mbao
kutoka mwanza kwa bao 2-0 katika mwendelezo wa ligi daraja la Kwanza.
Mchezo
huo ulichezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa, Oljoro
iliwachukua dakika 5 kupata bao la kwanza mara baada ya mchezo kupitia kwa
Laurence Milton, bao ambalo lilidumu kwa dakika 45 za mwanzo.
Mara
baada ya mapumziko Timu ya Mbao walikuja juu huku wakikosa mabao mengi, kutokana
na safu yao ya ushambuliaji kutokuwa makini katika eneo la hatari.
Hata
hivyo Mbao wakijua mchezo huo utakwisha hivyo walijikuta wakiongezewa kichapo
zikiwa zimesalia dakika 9 mchezo kuisha, bao lililofungwa na Abdala Bunu baada
ya kuwatoka walinzi wa Mbao na kufunga bao safi.
Hadi
mchezo una malizika Timu ya Mbao walijikuta wakiambulia Kadi sita za njano na
huku Lameck Daniel akiambulia kadi Nyekundu baada ya mchezo kuisha,ambapo
haikifahamika kosa alilolifanya.
Katibu
Mkuu wa Mbao Richard Atanas mara baada kumalizika mchezo aliwatupia lawama
waamuzi kwa kuwakandamiza katika mchezo huo.
“nimelazimishwa
kufungwa, Oljoro wapo nyumbani lazima wabebwe, wachezaji wangu wametolewa
mchezoni tangu kipindi cha kwanza haiwezekani kadi sita za njano na nyekundu
moja zinatolewa bila sababu za msingi kwa kweli maamuzi sio mazuru, na
sishangai mtu akiwa nyumbani lazima avune na ndivyo walivyofanya wenzetu”
alisema Atanas
Oljoro
wanafikisa Pointi 7 wakati Mbao wakisalia na Pointi 4, hivyo mchezo unaofuta Oljoro
wanaeleke Dodoma kukutana na JKT Kanembwa ya Kigoma, wakati Mbao watakua
nyumbani kuikaribisha Panone Fc ya Moshi ambayo katika mchezo wao mwishoni mwa
wiki walilazimishwa suruhu na Geita Goldern Star.
Naye
kocha msaidizi wa JKT Oljoro aliongeza kuwa watarajio yao ni kuendelea kufanya
vizuri na hatimaye kurejea ligi kuu msimu ujao hivyo sapoti kwa wadau
inahitajika zaidi.
Post a Comment