PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mbunge Deo Filikunjombe na baba yake Jerry Silaa wamefariki kwa ajali ya Helikopta.. #RIP
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kumekuwa na mvutano wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea j...



Kumekuwa na mvutano wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea jioni ya October 15 2015 katika Msitu wa Mbuga ya Selous, pembeni ya Mto Ruaha.
Jerry INSTA
Jerry Silaa amepost Ujumbe huu akithibitisha kufariki kwa Mbunge Deo Filikunjombe pamoja na baba yake, Mzee William Silaa ambaye alikuwa Rubani wa Helikopta hiyo >>> “Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani— jerrysilaa
Hii ni picha ya zamani, Mbunge Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.
Hii ni picha ya zamani, Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.
Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr. Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS>>> jerrysilaa
Deo Filikuonjome
Marehemu Deo Filikunjombe na baadhi ya Wapigakura wake wa Jimbo la Ludewa, Mkoa wa Njombe.
  Jerry Silaa lakini simu yake ilipokelewa na Msaidizi wake, Fadhili Idd ambaye amesema ni kweli wanethibitishiwa kuhusu taarifa ya Msiba na wanajiandaa na taratibu nyingine kwa sasa.
RIP Marehemu Captein William Silaa & Mbunge Deo Haule Filikunjombe.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top