Dk.
Umanath Nayak, mshauri mkuu wa magonjwa ya saratani ya kichwa na
shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya
saratani ya Apollo Hyderabad nchini India
Na Mwandishi Wetu,
Sekta
ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi yanayolenga kuongeza umri wa
kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi, njia bora za
matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya. Teknohama
imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii
muhimu. Makampuni yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa
yanalenga katika kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi
zaidi bila madhara makubwa kwa mgonjwa.
Kuna
matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti.
Teknolojia hii ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja
ya mambo muhimu yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa
upasuaji kwa kutumia roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu,
ambao hufanyika kwa shida, au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu
kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu inayopatikana katika
Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.
Mikono
ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia
mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule wa mchezo wa video,
maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa usahihi zaidi
wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa ikitumika
awali ya ‘laparoscopic’. Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina
hii unaweza kuondoa uvimbe uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia
humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya
muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na
tishu katika eneo husika.
Upasuaji
kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu hali mbalimbali kama vile
magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja kuondoa mfuko wa
uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani katika
mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids
uterine), saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi,
fistula na viungo katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed).
Utaratibu wa upasuaji na ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi
kupitia teknolojia hii. Kulingana na huduma ya afya inayoitajika na umri
wa mgonjwa, upasuaji kutumia Roboti pia unaweza kusaidia kuboresha afya
ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo wa kuzaa.
Kwa
wagonjwa wa saratani, mara nyingi upasuaji wa aina hii huusisha
upasuaji wa kichwa, shingo, ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake,
kuondoa uvimbe kwenye utumbo (colorectal surgery) na upasuaji
unaohusisha nyonga.
Mfumo
huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanahitaji
upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini ya shingo.
Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila
kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.
Dk
Umanath Nayak, mshauri mkuu wa wa magonjwa ya saratani ya kichwa na
shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti kutoka hospitali ya
saratani ya Apollo Hyderabad India ameelezea faida ya upasuaji kwa
kutumia Roboti. Anasema kuwa, "teknolojia ya kutumia Robot katika
upasuaji itadumu sana kama tunaweza kuona faida nyingi za teknolojia hii
ikilinganishwa na njia mbalimbali za zamani za upasuaji. Ni hatua ya
pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu huku ukiangalia kwenye
Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja ya kufanya
upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi "
Anaongeza kuwa, "Upasuaji
wa kutumia Robot ni njia mpya ya upasuaji ya isiyo na madhara na
inajumuisha upasuaji wa kawaida (Open surgery) na Upasuaji wa kutumia
skrini ya computer (laparoscopic). Kwa msaada wa Mikono maalumu ya Robot
inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya upasuaji kupitia mikato midogo
sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na makovu makubwa yatokanayo
na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu, maumivu baada ya
upasuaji na kupona kwa haraka zaidi ".
Aidha
mtaalamu wa magonjwa ya saratani nchini Dk. Harrison Chuwa, anasema
kuwa “upasuaji kwa njia ya roboti ni njia kuu ya kufanya upasuaji ambayo
itapunguza mapungufu ya kibinadamu na hata kovu la operesheni kuwa dogo
ambalo aliweze kufanya mwili wako kuonekana tofauti na ulivyokuwa
awali. Faida nyingine ya upasuaji kwa njia ya roboti ni kwamba unahitaji
rasimali kidogo ya binadamu ili kufanikisha kazi hii.
Teknolojia
ya roboti haipatikani nchini Tanzania, lakini watanzania wengi
wanasumbuliwa na saratani za kichwa na shingo na mfumo wa mkojo (mfano.
kibofu), uzazi, upasuaji wa utumbo mkubwa, na matatizo mengine wamepata
huduma hii mara kadhaa pale walipopata rufaa ya kwenda kutibiwa katika
hospitali za Apollo nchini India.
Ishara
nyingine nyingi bado zina mjadala kwa maana njia hii ni mpya tokea
upasuaji wa laparoscopic uanzishwe. Muda unavyosogea, upasuaji kwa njia
ya roboti unatarajiwa kuchukua nafasi za upasuaji wa kawaida wa saratani
na utakuwa ni msaada na kimbilio kwa wengi wanaoteseka na saratani na
mapungufu mengine. Inaweza tokea siku hapo baadae wakati daktari wa
upasuaji amekaa ofisini kwake na anamfanyia mgonjwa operesheni au
upasuaji akiwa mbali kwa msaada wa mfumo wa roboti.
Mwaka
jana, Hospitali Apollo mjini Apollo Chennai na Hyderabad imefanikiwa
kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna shaka
kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kifaa muhimu katika masuala ya
upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi
zinazoendelea.
Kuhusu Hospitali ya Apollo
Hospitali
za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za
upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji
isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo
hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa
wagonjwa.
Taasisi
ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika
utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu
bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci
inayotumika katika upasuaji.
Mfumo
huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa
yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake
(Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa
mgongo.
Post a Comment