‘Leo tarehe 29, October 2015 kupitia
Mgombea mwenza Mh, Juma Duni Haji aliwasilisha rasmi malalamiko kuhusu
mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi ‘ – Edward Lowassa
‘Tumeainisha kwenye malalamiko yetu
kutokuridhisha kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali hususani,
utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana
katika vituo vya kupigia kura kama ifuatavyo’ – Edward Lowassa
1.Upunguzwaji wa kura zangu
2.Kuongeza kura kwa wagombea wa CCM
3.Kuendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya
matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa demokrasia
kunaonekana wazi kutokana na mwenendo wa tume kuendelea kutangaza
matokeo yasiyo ya kweli kupora ushindi wetu
Aidha kumekuwepo pia na uporaji kwa wagombea Wa vyama vya Ukawa kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani.
‘Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu
sisi zilionesha kwamba nilikuwa naongoza kwa zaidi ya 67% na sasa
tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10, 268, 795 sawa na asilimia 62%
baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima kwa
hali hii, ninaitaka tume ya taifa ya Uchaguzi itangaze mara moja mimi
Edward Ngoyai Lowassa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania’ – Edward Lowassa
‘Tanzania kwa miaka mingi imefahamika
kama kisiwa cha Amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya
ulinzi na Usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita
mitaani kana kwamba uchaguzi ni vita hii ni kuwatisha wananchi ili
wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao
wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo’ – Edward Lowassa
Post a Comment