Mkurugenzi
wa Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Dr. Binadamu Hellen Bisimba
akizungumza na wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa ilani ya uchaguzi
ya Azaki Tanzania katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za binadamu na utawara bora,Bahame Nyanduga akizindua
ilani ya uchaguzi ya Azaki Tanzania katika ukumbi wa Milleniamu Towers
Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji
wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Hellen Bisimba na wakulia
Mratibu wa Mtandao wa watetea wa haki za Binadamu Onesmo Ngurumwa.
Wakionesha
waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya uzinduzi wa ilani ya
uchauzi ya Azaki katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyam
Jijini Dar es Salaam.
Bahame
Nyanduga na Dr. Binadamu Hellen wakiteta jambo mara baada ya uzinduzi
huo katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama Jijini Dar es
Salaam.
Sehemu
ya viongozi mbalimbali walio hudhulia uzinduzi huo katika ukumbi wa
Milleniamu Towers Kijitonyama Jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
VYAMA
vya Siasa vimeaswa kuachana na lugha ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa
amani na badala yake vimetakiwa kunadi sera zao kwa wananchi waweze
kupewa ridhaa inayotokana na kura.
Hayo
ameyasema Mwenyekiti wa Tume ya Haki ya binadamu na Utawala Bora,
Bahame Nyanduga wakati wa uzinduzi wa ilani ya Asasi za Kiraia
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Nyanduga amesema wakati wa sasa
ni kunadi sera kwa vyama vya siasa na sio kutumia lugha ambazo
haziendani na Demokrasia wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu.
Mwenyekiti
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora alitaja baadhi ya lugha
zinazotumika ni pamoja na Tutashinda saa Nne Asubuhi, Goli la Mkono zote
ni lugha ambazo hazitakiwi katika kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Amesema
kuwa vyombo vya dola ikiwemo jeshi la Polisi kuhakikisha linasimamia
wananchi katika mchakato wa kuelekea katika uchaguzi pasipo kutumia
nguvu ili wananchi waweze kusikiliza sera za vyama vyote kupitia
wagombea wake.
Hata
hivyo amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zilizosaini kuwepo kwa
Mahakama ya ICC hivyo wale wote ambao watashiriki kuvunja amani wakati
wa uchaguzi mkuu watahusika na mahakama hiyo kutokana na kufanya
uchochezi na kuvuruga amani.
Aidha
amesema kuwa wananchi nao wametakiwa kuvumiliana katika kipindi hiki
pasipo kudharau chama cha mwenzake, uchanaji wa mabango ya wagombea
kwani hiyo sio demokrasia.
Post a Comment