PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TIMU YA POLISI, CDTI WAENDELEA KUKOLEZA MOTO.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. PrincemediaTZ Timu za netiboli za Polisi na CIDT za jijini hapa ambazo zinatarajia kwenda katika mashindano ya k...
NA; YOHANA CHALLE. PrincemediaTZ


Timu za netiboli za Polisi na CIDT za jijini hapa ambazo zinatarajia kwenda katika mashindano ya klabu Bingwa Tanzania yanayofanyika mkoani Shinyanga kuanzia septemba 14 hadi 26 mwaka huu zimeendele na mazoezi ili kuhakikisha zinaenda kufanya vizuri.

Akizungumzia juu ya maandalizi ya timu ya Polisi kocha mkuu wa timu hiyo Joseph Lameck alisema kuwa tayari wachezaji wake wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya kwenda kupandana katika ligi hiyo.

“wachezaji wanaendelea vizuri na ninamshukuru Mungu hakuna majeruhi hadi hivi sasa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mapambano na wanamori ya mashindano na tunasubiri kuondoka” alisema Lameck.

Aliongeza kuwa wachezaji bado wapo kambini na wanafanya mazoezi asubuhi na jioni ili kuendelea kujiweka fiti zaidi kutokana na ushindani mkubwa ambao wanaupata katika mashindano hayo.

“nawahaidi wapenzi wa netiboli kuwa ushindi lazima kwani tangu tupande daraja hatujawahi kushuka hivyo wasiwe na wasiwasi na hilo kwa kuwa timu zote zinazoshiriki tunazifahamu vizuri na hatuoni wa kutuzuia japo najua ushindani utakuwepo” aliongeza kusema Lameck.

Zaidi ya timu 15 zinatarajia kushiriki katika mashindano hayo kutoka mikoa mbalimbali ambapo kati ya hizo timu nne zitachaguliwa kwenda katika mashindano ya Muungano ambapo huko nako watampata bingwa atakaye iwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.  

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top