Na; YOHANA CHALLE. PrincemediaTZ
Timu ya maafande wa Jkt Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza
Tanzania bara inatarajia kuchuana vikali na ndugu zao AFC katika ufunguzi wa
ligi maalum ya Nyerere Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi septemba 10 jiji
hapa.
Tayari timu ya zote zimethibitisha kushiriki michuano hiyo huku
kila mmoja akijitamba kuonyesha ubabe dhidi ya mwenzake na pia wakitumia mechi
hiyo kutambulisha wachezaji waliosajiliwa kwa wapenzi wa Soka wa jiji Arusha.
Mechi hiyo ya ufunguzi kati ya Oljoro na AFC
itakayochezwa katika uwanja wa Sheik Amri Abeid, ni kwa ajili ya
kufungua michuano ya Nyerere Cup itakayoshirikisha Jumla ya timu Sita za
vijana chini ya umri wa miaka 13, lengo kubwa ikiwa ni kumuenzi muasisi wa
Taifa hili Hayati Mwl, Julius K. Nyerere.
Akizitaja timu shiriki katika mashindano hayo, mratibu wa
maadhimisho hayo Bertha Ismail alisema kuwa ni pamoja na Nyota Accademy, Future
Star, Kijenge Youth zingine ni Rolling stone, Young Life na Pallot.
“Maadhimisho hayo huwa yanafanyika kila Octoba 14 kila mwaka
lakini kwa mwaka huu tunafanya mwezi Septemba ili maadhimisho haya yasiathiriwe
na zoezi la Uchaguzi ambapo pamoja na kumuezi Muasisi wa Taifa letu lakini mashindano
haya pia inalenga kuhamasisha wananchi wafanye uchaguzi kwa amani bila vurugu
ili sekta ya utalii hapa nchini izidi kukua” alisema Ismail
Post a Comment