NA; YOHANA CHALLE. PrincemediaTZ
Timu za netiboli
za Polisi na CIDT za jijini hapa ambazo zinatarajia kwenda katika mashindano ya
klabu Bingwa Tanzania yanayofanyika mkoani Shinyanga kuanzia septemba 14 hadi
26 mwaka huu zimeendele na mazoezi ili kuhakikisha zinaenda kufanya vizuri.
Akizungumzia
juu ya maandalizi ya timu ya Polisi kocha mkuu wa timu hiyo Joseph Lameck alisema
kuwa tayari wachezaji wake wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya kwenda
kupandana katika ligi hiyo.
“wachezaji
wanaendelea vizuri na ninamshukuru Mungu hakuna majeruhi hadi hivi sasa wachezaji
wapo tayari kwa ajili ya mapambano na wanamori ya mashindano na tunasubiri
kuondoka” alisema Lameck.
Aliongeza kuwa
wachezaji bado wapo kambini na wanafanya mazoezi asubuhi na jioni ili kuendelea
kujiweka fiti zaidi kutokana na ushindani mkubwa ambao wanaupata katika
mashindano hayo.
“nawahaidi
wapenzi wa netiboli kuwa ushindi lazima kwani tangu tupande daraja hatujawahi
kushuka hivyo wasiwe na wasiwasi na hilo kwa kuwa timu zote zinazoshiriki
tunazifahamu vizuri na hatuoni wa kutuzuia japo najua ushindani utakuwepo”
aliongeza kusema Lameck.
Zaidi ya
timu 15 zinatarajia kushiriki katika mashindano hayo kutoka mikoa mbalimbali
ambapo kati ya hizo timu nne zitachaguliwa kwenda katika mashindano ya Muungano
ambapo huko nako watampata bingwa atakaye iwakilisha Tanzania katika mashindano
mbalimbali ya kimataifa.
Post a Comment