PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CHAMA CHA NGUMI ZA RIDHAA AABA KUFANYA MKUTANO MKUU JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Chama cha ngumi za ridhaa mkoani hapa (AABA),kinategemea kufanya mkutano mkuu muda wowote kuanzi...



NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Chama cha ngumi za ridhaa mkoani hapa (AABA),kinategemea kufanya mkutano mkuu muda wowote kuanzia sasa ili kuweka mikakati ya chama hicho kwa miaka mitano ya baadae.

Akizungumza na gazeti hili katibu mkuu wa AABA Mohamed Abubakari, alisema kuwa wapo katika hatua za mwisho kukutana na wadau mbali mbali wa ngumi wa kutoka mkoani hapa na wengine nje ya Arusha ili kukiimalisha chama kwa faida ya vizazi vijavyo.

“tunahitaji kuweka mipango kazi ya miaka mitano ijayo kuanzia sasa, ili kukiimalisha zaidi chama, na kuongeza nguvu kazi hasa kwa vijana ambao wataitangaza Arusha kwa siku za mbele” alisema Abubakari.

Aliongeza kuwa baada ya mkutano huo AABA hakitashiriki mashindano yoyote nje ya mkoa wa Arusha kwa miaka miwili mfululizo ili kuwapima na kuwaivisha vijana wao.

“wachezaji watakao toka kushiriki mashindano nje ya Mkoa waetu ni wale waliokuwa kwenye timu ya taifa pekee, hawa wengine hatutawaruhusu hadi watakapo kuwa wameiva vizuri katika miaka hiyo miaka miwili” aliongeza kusema Abubakari.

Aliongeza kuwa ndani ya miaka miwili AABA watakuwa wameanzisha kliniki mbalimbali za mchezo wa ngumi pamoja na kufanya matamasha mengi ili kuwahamasisha watoto wadogo.

Katibu huyo alitoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kuwaruhusu vijana wao kushiriki mchezo huo akisema kuwa ni mchezo wenye faida kubwa ikiwa pamoja na ajira na ulinzi wa afya zao.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top