PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NSSF YATOA MSAADA WA SH.10 MILIONI ZA UKARABATI WA SHULE ARUMERU MAGHARIBI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mbunge wa Arumeru Magharibi mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye akiinua juu mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.10 milioni iliyotolewa na mf...





Mbunge wa Arumeru Magharibi mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye akiinua juu mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.10 milioni iliyotolewa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF kwaajili ukarabati wa Shule ya Msingi Sekei,Kata ya Sokon II iliyoanzishwa miaka 70 iliyopita.




Mbunge wa Arumeru Magharibi mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.10 milioni iliyotolewa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF kwaajili ukarabati wa Shule ya Msingi Sekei,Kata ya Sokon II iliyoanzishwa miaka 70 iliyopita,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha,Fidelis Lumato.




Diwani wa Kata ya Sokon II wilaya ya Arumeru,Kendo Laizer akizungumza kwenye mkutano huo na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada wa wadau wengine kwa kuchangia ukarabati wa Shule hiyo.


Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)Jackton Ochieng akizungumza katika hafla .



Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sekei wakishangilia baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na vifaa mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya Shule hiyo.




Mbunge wa Arumeru Magharibi mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa NSSF ,viongozi mbalimbali na walimu wa Shule za Sekei na Naurei.




Na Mwandishi Wetu,Arumeru
Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa NSSF umetoa msaada wa Sh.10 milioni kwaajili ya kukarabati Shule ya Msingi kongwe ya Sekei inayotimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake.


Akikabidhi mfano wa hundi hiyo leo,Meneja Uendeshaji wa NSSF mkoa wa Arusha,Jackton Ochieng amesema wametoa mchango huo kutokana na kutambua umuhimu wa elimu katika jamii.


Pia amewataka wananchi kujifunza namna mifiko ya hifadhi ya jamii inavyofanya kazi zake ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo ya Elimu,Uzazi,Mazishi,Kuumia kazini na mengine.


Kwa upande wake Mbunge wa Arumeru Magharibi,Godluck Ole Medeye alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Dk Ramadhan Dau kwa kukubali kuchangia ukarabati wa Shule hiyo ambayo ni ukombozi kwa jamii ya eneo hilo.


"Ili tuwe na taifa endelevu hatuna budi kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia ili tujihakikishie kuwa na wataalamu katika fani mbalimbali ambazo ni msingi wa maendeleo."amesema Ole Medeye


Katika hatua nyingine mbunge huyo amewahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la makzi ili kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top