NA; YOHANA CHALLE.
MOSHI.
Timu ya Panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu
kama matajiri wa mafuta ,inaahidi kuendeleza kichapo kwa kila timu inayokutana
nayo katika ligi daraja la kwanza iliyoanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki.
Panone katika mchezo
wake wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa ushirika mjini mshi dhidi ya JKT Oljoro
waliibuka na ushindi wa bao 4-0 na kuweka matumaini ya kufanya vizuri zaidi
katika ligi hiyo.
Msemaji wa timu hiyo
Husein Mwinyi alisema kuwa kwa sasa timu hiyo wanajiandaa kuchukua alama tatu
nyingine mwishoni mwa wiki watakapoikaribisha timu ya Polis Tabora
“Licha ya kupata
ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Oljoro bado kocha hajalidhika na
wachezaji wake kutofuata maelezo hasa katika eneo la katikati wachezaji
walikuwa hawaelewani vizuri” alisema Mwinyi.
Mara baada ya mchezo
wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Polis Tabora, Panone FC itaelekea mjini Kigoma
kupambana na JKT kanembwa.
Hadi sasa Pnone ndio
wanaoongoza kundi C kwa kujikusanyia alama tatu na mabao 4, huku Polis Tabora wakifuatia
wakiwa na alama tatu na mabao matatu.
Post a Comment