NA, YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Mara baada ya kupokea kichapo cha
mabao 4-0 mwishoni mwa wiki dhidi ya Panone, Oljoro inajiandaa kuelekea Tabora
mwishoni mwa wiki kucheza na Rhino
Rangers katika mwendelezo wa ligi daraja la kwanza.
Katibu mkuu wa Oljoro Husein Nalinga
alisema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa
general Tyre njiro kulingana na ratiba ya kocha.
“kocha mkuu wa timu bado ni mgeni hana
hata mwezi na bado hajawazoea wachezaji vizuri, lakini anawahaidi wapenzi na
mashabiki wa Oljoro kulekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita
dhidi ya Panone” alisema Nalinga.
JKT Olojro ipo katika kundi ‘C’ pamoja na timu za Panone ,Polisi Mara –Mara,Rhino Rangers –Tabora,Mbao
fc –Mwanza,Polisi Tabora -Tabora,Geita Gold –Geita na JKT Kanembwa
– kigoma.
Timu hiyo ndio tegemeo
kwa wakazi wa Arusha ili kuhakikisha wanapata timu itakayoshiriki ligi kuu
Tanzania Bara msimu ujao, kwani tangu AFC inayoshiriki ligi daraja la Pili na Oljoro
zishuke daraja wakazi wa Mkoa huu hawajashuhudia timu yoyote kubwa ilikuja
kucheza mchezo hata wa kirafiki.
Nalinga aliongeza kuwa
licha ya kupoteza mchezo wa kwanza bado timu hiyo inweza kurudi ligi kuu kwa
kuwa ligi bado mbichi na watajipanga na kufanya vizuri zaidi.
Post a Comment