CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.
Na Modewjiblog team
Mfanyabiashara
Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya
Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha
tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015)
amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group,
hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia
kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.
Dewji
maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa
moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha
BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.
Kupitia
kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia
ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Ambapo
ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba
yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.
Aidha,
MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo
midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.
Salim
Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda
kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:
“Unajua
na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa
mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk
nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani,
benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki
za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo
la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa
mtu mwenye pesa. alifafanua MO .
Katika
mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL
GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya
24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya
Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.
Tuzo
aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli
ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu
wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive
Masiyiwa na Helen Hai.
MO
alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania
tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine
walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor
Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar
Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
Post a Comment