PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JUMLA YA EKARI 7000 KUGAIWA KWA WANANCHI 2000 WA ARUSHA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Serikali imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya Tanzania plan...




Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Serikali imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya Tanzania plantatition limited yaliyokua yakimilikiwa na mwekezaji  kutoka nje ,mashamba hayo yanatajiwa kugawanywa kwa wananchi 2000 wenye uhitaji wa ardhi ya makazi na mashamba .

Aidha baada ya ubatilishwaji wa mashamba hayo Arusha imepata ekari 6176.5 na Halmashauri ya Meru ekari 925  hivyo kufikia ekari 7101 ambazo zitagawanywa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi,Wiliam Lukuvi wakati akitoa taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi  katika mikoa ya Arusha na Manyara katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,Lukuvi amesema kuwa mashamba hayo yalikua na migogoro kwa kipindi kirefu kati ya mwekezaji na Wananchi hivyo kutokana na uhitaji mkubwa wa ardhi serikali imeamua kubatilisha mashamba hayo.

“Nimekuja Arusha na timu yangu ambayo itafanya uhakikiki wa watu 2000 wenye uhitaji na baada ya kujiridhisha watafanya zoezi la ugawaji na pia wananchi watapatiwa hati ya kumiliki ardhi zao safari hii hatutagawa ardhi kienyegi” Alisema Lukuvi

Lukuvi amesema kuwa mbali na shamba hilo pia wamepata ekari 100 katika shamba la Imani Estate na pia Shamba la Noors  lenye Ekari 2296  lililokua na mgogoro kati ya Mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha Laroi na Kisima cha Mungu litagaiwa kwa wananchi baada ya mazungumzo kati ya Mwekezaji kukubali kuachia shamba hilo


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC ,Fidelis Lumato amesema kuwa ugawanywaji wa mashamba hayo utasaidia kupunguza migogoro mikubwa ya ardhi iliyokua inakabili wilaya hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa ardhi.

Jumla ya migogoro 80 iliyowasilishwa kwa Waziri Lukuvi kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Meru imepatiwa ufumbuzi hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ilikua ikilisakama jiji la Arusha.





About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top