PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: GOFU ARUSHA YAENDELEA KUNOA WACHEZAJI. ILI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA KIMATAIFA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE.PrincemediaTZ   Klabu ya gofu ya Arusha Gymkhana (AGC), imeendelea na mashindano yake ya kila mwisho wa mwezi a...

NA; YOHANA CHALLE.PrincemediaTZ
 
Klabu ya gofu ya Arusha Gymkhana (AGC), imeendelea na mashindano yake ya kila mwisho wa mwezi ambapo Simon Travers imeshinda kwa alama za Division ‘A.

Katika mashindano yaliyofanyika  mwishoni mwa mwezi uliopita (mwezi wa nane), katika viwanja vya gofu vya Gymkhana Arusha yalimshuhudia mchezaji  Saimon Travers akiibuka mshindi kwa Division ’ A ‘ baada ya kupata  69 nett (lowest gross score) huku mshindi wa pili akiwa ni Isaac Wanyeche aliyepata  70  nett.

Kwa Divison ‘B’ Prabvir Singh aliongoza baada ya kujipatia  68 nett  akifuatiwa na Hussein Kermali ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya AGC aliyepata 72 nett,huku Division ‘C’ Kassim Somji  akijipatia 74 nett alizopata kwa ‘count back’ na mshindi wa pili kuwa ni Haja Modhwadia kwa 74 nett.

Pia michuano hiyo iliambatana na washindi wengine   ‘two club winners ‘ ambao ni Kush Lodhia ,Abby  Omary,Aayush  Nathwani, Isaac  Wanyeche , Muzzafar Yusufali ,na Gelase Ruta nao  pia walijipatia zawadi  mbalimbali  .

Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya wachezaji 37 , na hufanyika kila mwezi yakiwa na lengol la kuwafanya wachezaji wa klabu ya Arusha Gymkhana kuwa katika hali ya kimchezo wakati wote wa mashindano mbalimbali yanapotokea ndani na nje ya klabu .

“Sisi kama klabu tumejiwekea utaratibu wa kufanya mashindano kila mwisho wa mwezi ili tuweze kuwa tayari katika kuhakikisha mchezo huu wa gofu kupitia wachezaji wa Arusha Gymkhana  tunakuwa na uwezo wa kipekee utakaotuwezesha tuweze kuonyesha ushindani wa aina yake katika mashindano tofauti tofauti yatakayokuwa yanafanyika”aliongeza Bandali.

Aidha klbu hiyo ya Arusha Gymkhana inatarajia kufanya mashindano yake mengine yatakayofanyika jumamosi ya tarehe  12 septemba jijini hapa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top