PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ASILIMIA 50% YA WAHITIMU WA VYUO HAWAKIDHI SOKO LA AJIRA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Asilimia 50% ya wahitimu kutoka vyuo vikuu hawakidhi mahitaji ya soko la Ajira katika nchi za ...


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Asilimia 50% ya wahitimu kutoka vyuo vikuu hawakidhi mahitaji ya soko la Ajira katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hali inayopelekea Wahitimu wengi kutoajiriwa katika sekta binafsi na zile za serikali.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Baraza la Vyuo Vikuu vya  Afrika Mashariki (IUCEA)  pamoja na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC ) mwaka 2013 hadi mwaka 2014  uliohusisha Waajiri kutoka mashirika binafsi na yale ya serikali ,Waajiri  wengi walilalamikia juu ya Wahitimu wanaozalishwa na vyuo kutokidhi haja ya soko la ajira.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyuo vikuu vya Afrika Mashariki,Profesa Mayunga Nkunya alisema kuwa changamoto zilizooainishwa katika utafiti huo  na waajiri ni pamoja na wahitimu kutoweza kutumia maarifa waliyoyapa kuleta tija katika maeneo ya kazi,kuwa na elimu ya nadharia kuliko ya vitendo pamoja na kukosa ujasiri wawapo kazini.

Profesa Mayunga aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari juu ya Kongamano kubwa la kuwakutanisha waajiri,Wafanyabiashara na Wanafunzi wa Vyuo litakalofanyika nchini Uganda Octoba mwaka huu  lengo ni  kujadili mambo muhimu ambayo yanaweza kusaidia kuboresha elimu ya vyuo iweze kukidhi matakwa ya soko la ajira.

Mayunga alisema kuwa badala ya waajiri kulaumu wanayo nafasi ya kushiriki katika kutoa mawazo ambayo yatasaidia katika kuwaandaa wahitimu waweze kuleta matokeo yanayotarajiwa katika jamii.

“Waajiri wengi hulalamikia mitaala yetu kuwa haiendani na hali halisi ya soko mingine imeangalia mahitaji ya miaka ya nyuma na si sasa hiyo ni changamoto ambayo inapaswa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu” Alisema Profesa Mayunga

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) ,Lilian Awinja alisema kuwa kutokana na ugunduzi wa mafuta na gesi unaoendelea katika ukanda wa Afrika Mashariki vyuo vikuu vina jukumu la kuwaandaa wahitimu wawe na ujuzi unaohitajika katika sekta hiyo badala ya kuchukua wataalamu kutoka nje.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top