NA
YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ
Chuo cha uandishi
wa habari na Utangazaji Arusha (AJTC) mwishoni mwa wiki kimefanikiwa kutwaa
ubingwa wa mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari
za michezo mkoani Arusha (TASWA)
Mashindano hayo
yaliandaliwa kwa lengo ikiwa kuhamasisha uchaguzi wa amani,huru na wa haki
hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa
Urais,Wabunge na madiwani.
Mashindano hayo
yalichezwa kwa mfumo wa ligi na AJTC walitwaa ubingwa kwa kufikisha
pointi 7 wakifuatiwa na ORS Radio ya Manyara ilikuwa na pointi 4.
Pamoja na AJTC na
ORS Radio timu nyingine zilizoshiriki ni TASWA Dar es salaam, TASWA Arusha, MJ
radio, na Arusha One FM.
Mwenyekiti wa
TASWA ,Musa Juma alizipongeza timu zote kwa ushiriki wao hasa katika kipindi
hiki ambacho Taifa letu lina elekea katika uchaguzi mkuu mwezi wa kumi mwaka
huu.
“napendsa
kuwasihi waandishi wenzangu na wananchi wote kuhakikisha wanapiga kura na
kumchagua kiongozi atakaye leta maendeleo na kuwajari watanzani bila kubagua”
alisema Juma.
Aliongeza kuwa
waandishi wanahitajika kutumia vizuri kalamu zao katka kuwaelimisha wananchi
juu yauchaguzi hna sio kuwapamba wagombea kwenye vyombo vya habari.
Post a Comment