NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ
Timu ya AFC
inayojiandaa kushiriki ligi daraja la pili (SDL) Tanzania Bara, katikati ya
wiki walionesha kazi mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa Shekh Amri Abeid
walipokutana na Kaka zao JKT Oljoro na kutoshana nguvu kwa kufungana Bao 1 – 1.
Mchezo huo
ulikuwa maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano yaliyoandaliwa kwa ajili ya
kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwali Julias Kambarage Nyerere.
Oljoro ndio
walikua wa Kwanza kujipatia bao kwa njia ya mkwaju wa penati kupitia mchezaji
wao Lukas Charles mnamo dakika ya 62, wakati AFC walisawazisha dakika ya 78
kupitia Malechela Mndima baada ya kuitoka ngome ya Olojo.
Afisa elimu
wa jiji la Arusha Josephat Ntabindi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi
wa mashindano hayo alipenda kuwasihi wachezaji na timu zote zinazoshirki
kuhakikisha wanaanya juhudi ili kurudisha hadhi ya jiji katika michezo
“mkoa wetu
unahitaji jitihada za ziada ili kuhakikisha mwakani tunakuwa na timu
inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara,nah ii yote tutafanikiwa endapo
tutashirikiana kwa pamoja” alisema Ntabindi.
Kwa sasa
wakazi wa arusha wanaingalia JKT oljorokama mkombozi wao atakayewafuta aibu
hiyo, Oljoro inashiriki Ligi daraja la kwanza (FDL) wakatitimu ya AFC na Mdini
zikiwa zinashiriki ligi daraja la pili (SDL).
Mashondano
ya Nyerere Cup yameamnadiliwa kwa lengo la Kumuenzi Mwalimu pamoja na kutangaza
utalii wa ndani hasa mlima Kilimanjaro na yatafika tamati septemba 19 mwaka huu.
Bertha
Ismail ambaye nimratibu mkuu wa maadhimishohayo alisema kuwa timu shiriki
katika mashindano hayo, hayo ni pamoja na Nyota Accademy, Future Star, Kijenge
Youth zingine ni Rolling stone, Young Life na Pallot
“Maadhimisho
hayo huwa yanafanyika kila Octoba 14 kila mwaka lakini kwa mwaka huu tunafanya
mwezi Septemba ili maadhimisho haya yasiathiriwe na zoezi la Uchaguzi ambapo
pamoja na kumuezi Muasisi wa Taifa letu” alisema Ismail
mashindano
haya pia yanahamasisha wananchi wafanye uchaguzi kwa amani bila vurugu ili
sekta ya utalii hapa nchini izidi kukua.
Post a Comment