Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wanawake Wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya Tanga,Singida
,Manyara na Morogoro wameiomba serikali ipunguze ada ya leseni ya uchimbaji
madini ili kuwawezesha kinamama wanaoanza kazi hiyo wasikwame kiuchumi
kutokana na kukabiliwa na changamoto ya bei kubwa ya vifaa vya uchimbaji pamoja
na ukosefu wa mitaji.
Kinamama hao ambao wameamua kujikita kwenye shughuli za
uchimbaji wa madini wameiomba serikali
isikie kilio chao cha muda mrefu licha ya sekta hiyo ngumu bado
inawasaidia kinamama kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Pili Hussein ni mwanamama wa kwanza kuzama katika migodi ya
Mirerani na kuchimba madini ambaye kwa sasa ni mmiliki wa kitalu cha madini
amesema kuwa gharama kubwa za uendeshaji wa
migodi zimekua zikirudisha nyuma juhudi za kinamama hivyo ameiomba
serikali na mashirika binafsi kujitokeza kuwasaidia kinamama kupata mikopo
itakayoiwasaidia kuendesha shughuli za uchimbaji
Wakizungumza katika jukwaa la kinamama wachimbaji wa madini
linaloendelea mkoani Kilimanjaro
lilioandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Hakimadini ,jukwaa lenye lengo la kuunganisha sauti na
nguvu ya kinamama katika kutetea haki zao hususan katika sekta ya madini na kunufaika ipasavyo,Mwansy Shomari ni
Mchimbaji wa Madini aina ya Ruby kutoka eneo la Kalalani mkoani Tanga amesema kuwa licha ya changamoto
wanazozipitia mfumo dume umekua ukiwakwamisha kinamama kupiga hatua kiuchumi
hususani katika sekta ya madini iliyotawaliwa na mfumo dume kwa kipindi kirefu
Kwa upande wake
Meneja Programu wa Shirika la Hakimadini ,David Ntiruka amesema kuwa
wameanzisha program maalumu ya kukusanya sauti ya kinamama wachimbaji pamoja na
changamoto zao ili kuzifikisha kwenye vyombo husika viweze kufanyiwa kazi
Mwamko wa wanawake
kujihusisha na shughuli za uchimbaji madini bado unakua na kuongezeka
ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo wanawake wachache walithubutu
kujihusisha na uchimbaji ,kutokana na kuongezeka kwa uelewa juu ya haki ya
kunufaika na madini kwa jinsia zote wanawake wengi wanashiriki katika uchimbaji
madini.
Post a Comment