PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WANAWAKE WACHIMBAJI MADINI WAIOMBA SERIKALI IPUNGUZE ADA YA LESSENI.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na   Ferdinand Shayo,Arusha. Wanawake Wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya Tanga,Singida ,Manyara na Morogoro wameiomba seri...



Na  Ferdinand Shayo,Arusha.

Wanawake Wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya Tanga,Singida ,Manyara na Morogoro wameiomba serikali ipunguze ada ya leseni ya uchimbaji madini  ili kuwawezesha kinamama  wanaoanza kazi hiyo wasikwame kiuchumi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya bei kubwa ya vifaa vya uchimbaji pamoja na ukosefu wa mitaji.

Kinamama hao ambao wameamua kujikita kwenye shughuli za uchimbaji wa madini wameiomba serikali  isikie kilio chao cha muda mrefu licha ya sekta hiyo ngumu bado inawasaidia kinamama kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Pili Hussein ni mwanamama wa kwanza kuzama katika migodi ya Mirerani na kuchimba madini ambaye kwa sasa ni mmiliki wa kitalu cha madini amesema kuwa gharama kubwa za uendeshaji wa  migodi zimekua zikirudisha nyuma juhudi za kinamama hivyo ameiomba serikali na mashirika binafsi kujitokeza kuwasaidia kinamama kupata mikopo itakayoiwasaidia kuendesha shughuli za uchimbaji

Wakizungumza katika jukwaa la kinamama wachimbaji wa madini linaloendelea  mkoani Kilimanjaro lilioandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Hakimadini  ,jukwaa lenye lengo la kuunganisha sauti na nguvu ya kinamama katika kutetea haki zao hususan katika sekta ya madini  na kunufaika ipasavyo,Mwansy Shomari ni Mchimbaji wa Madini aina ya Ruby kutoka eneo la Kalalani mkoani Tanga   amesema kuwa licha ya changamoto wanazozipitia mfumo dume umekua ukiwakwamisha kinamama kupiga hatua kiuchumi hususani katika sekta ya madini iliyotawaliwa na mfumo dume kwa kipindi kirefu


Kwa upande wake Meneja Programu wa Shirika la Hakimadini ,David Ntiruka amesema kuwa wameanzisha program maalumu ya kukusanya sauti ya kinamama wachimbaji pamoja na changamoto zao ili kuzifikisha kwenye vyombo husika viweze kufanyiwa kazi


Mwamko wa wanawake kujihusisha na shughuli za uchimbaji madini bado unakua na kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo wanawake wachache walithubutu kujihusisha na uchimbaji ,kutokana na kuongezeka kwa uelewa juu ya haki ya kunufaika na madini kwa jinsia zote wanawake wengi wanashiriki katika uchimbaji madini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top