Kiungo
hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiondika na mpira huku Mabeki wa
Timu ya Gor Mahia wakiangalia namna ya kumdhibiti, katika
mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015,
uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC
imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
Wachezaji
John Bocco (Azam) na Collins Okoth (Gor Mahia) wakiwa chini huku
wakiendelea kuonyesha umahiri wao wa kuucheza mpira hapa wakiwa
wamelala, wakati wa mtanange wa
fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao
2-0 na kutwaa ubingwa huo.
Beki
wa Timu ya Azam FC, Agrey Morris (13) akiondoa hatari iliyokuwa
ikielekezwa langoni mwao na Mshambuliaji wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya,
Godfrey Walusimbi.
Wanakosa goli pale hawa Gor Mahia...........
Kiungo
wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akionyesha uwezo wake
mbele ya Mshambuliaji Machachari wa timu ya Azam FC, Kipre Tchetche,
wakati wa mtanange wa fainali ya
Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja
wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa
ubingwa huo.
Sasa ni Kipre Tchetche na Karim Nizigiyimana.
kiungo wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akiachua shuti kuelekea lakongoni mwa timu ya Azam FC.
Kiungo hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiruka juu kuwania mpira dhidi ya Mshambuliaji wa Gor Mahia, Michael Olunga.
Washabiki wa Azam FC wakiishangilia timu yao.
Erasto Nyoni wa Azam FC akionyeshana uwezo na Kagere Medie wa Gor Mahia wakati wa mtanange
wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao
2-0 na kutwaa ubingwa huo.
Mpiga picha akiendelea kuchukua taswira mbali mbali za mtanange huo.
Washabiki wa Timu ya Gor Mahia wakionekana kuhuzunika baada ya timu yao kushindwa kufua dafu mbele ya wanalambalamba wa Azam FC.
Azam ni shangwe tupu.
Post a Comment