Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” katika pozi.
Mwandishi
wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu
kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu
wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo
jipya la Ushetu wilayani Kahama.
Mwandishi
wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu
kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu
wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo
jipya la Ushetu wilayani Kahama.
Mwandishi
wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu
kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akitangaza nia kuwania ubunge katika
jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama.
Mwandishi
wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu
kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akizungumza na wakazi wa Ushetu wakati
wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la
Ushetu wilayani Kahama.
Mwandishi
wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu
kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwajibika katika kazi yake ya
uandishi wa habari.
Mwandishi
wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu
kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa katika moja ya mikutano muhimu.
Na Mwandishi wetu
Siku
moja tu baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania kutangaza majimbo
mapya ya Uchaguzi,Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa
William Bundala maarufu kwa jina la “Kijukuu cha Bibi K” ametangaza
rasmi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge katika Jimbo la
jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani
Shinyanga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Bundala
ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili
aweze kupeperusha bendara ya Chadema/UKAWA katika uchaguzi mkuu ujao
katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha
Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.
Mtia
nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda
Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika
jimbo hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu
kama anavyotakiwa Mbunge Kufanya.
Alisema
kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo
ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania maendeleo ya
wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na
watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za wilaya.
Sambamba
na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea
wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo
hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi kutokana na asilimia kubwa
ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya
wana ushetu kama anavyoyafahamu yeye.
Aliongeza
kuwa akifanikiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo
jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la
saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la
ukosefu wa ajira kwa vijana.
Bundala
alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia
na kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika
kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa
Ardhi,Mirathi,haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na
mali zao kwa ujumla.
Akizungumzia
kuhusu suala la michezo katika jimbo hilo, Bundala alisema kuwa kupitia
Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa
michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi
kuu Tanzania Bara.
Awali
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu
Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana
mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge
wa jimbo hilo.
Wilaya
ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za
Msalala,halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na
kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.
Katika
kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi
ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA
wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana.
Post a Comment