Mwanachama wa CHADEMA Monduli mjini akiwa ambeba bango lenye ujumbe unaoashiria kumkaribisha Edward Lowassa katika chama hicho,jana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Monduli Mjini.Picha na Ferdinand Shayo |
Na Ferdinand Shayo,Monduli
Siku chache baada ya Lowasa kuenguliwa kwenye kinyang`anyiro cha
Uraisi kwa tiketi ya CCM,jana CHADEMA imezuru katika jimbo hilo na
kufanya mkutano wa hadhara ambapo wamepokea wanachama wapya 10
waliojiunga kutoka CCM.
Katika Mkutano huo uliobeba ujumbe wa Kumkaribisha Lowasa katika chama
hicho kwani bado milango haijafungwa kwa yeye kutimiza azma yake ya
kuwatumikia watanzania walio wengi
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)
,Happiness Chale alisema kuwa uamuzi mbaya walioufanya CCM Lowassa
hana budi kujiunga na CHADEMA mapema kabla milango haijafungwa ili
aweze kufanikisha azma yake ya kuwatumikia Watanzania.
“Saa ya ukombozi imefika wananchi wa Monduli wajiunge na chadema ili
kuleta mabadiliko na ukombozi wa kweli walioukosa kwa muda mrefu”
Alisema Happiness
Katibu wa BAWACHA ,Cecilia Ndossy ambaye pia ni Mtia nia katika jimbo
la Monduli amesema kuwa kwa kosa walilolifanya CCM hawapaswi kupewa
ridhaa ya kuongoza wananchi hao badala yake wachague chadema mahali
ambapo sauti ya watu inaheshimiwa na kupewa kipaumbele.
Cecilia amejizatiti kuhakikisha kuwa anaboresha huduma za afya,maji
safi na salama na miundombinu kwani jimbo hilo linakabiliwa na uhaba
mkubwa wa maji kwa muda wa miaka mingi.
Post a Comment