Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akibadilishana hati ya
mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Maxcom Africa,
Juma Rajabu baada ya uzinduzi wa huduma za ‘FahariHuduma wakala’ kupitia
vituo
vya Maximalipo. Hafla imefanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na
Francis
Dande)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Mkurugenzi wa Maxcom Africa,
Juma Rajabu wakisaini hati ya
mkataba wa makubaliano wa huduma za ‘FahariHuduma wakala’ kupitia
vituo
vya Maxmalipo.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na
Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akisaini hati ya
mkataba wa makubaliano wa huduma za ‘FahariHuduma wakala’ kupitia
vituo
vya Maxmalipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifurahia jambo na Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na
Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizugumza wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
BENKI ya CRDB na kampuni ya Maxcom Africa, imeingia mkataba
wa makubaliano utakaowezesha wakala wa Maxmalipo kutoa huduma za benki hiyo
kupitia mfumo wa fahari huduma.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa benki ya
CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema makubaliano waliyoyafikia yatasaidia benki
hiyo kutumia mtandao wa mawakala wa maxmalipo kutoa huduma kwa wateja
kiurahisi.
Alisema lengo la makubaliano hayo ni kupanua wigo wa kutoa
huduma ili kuweza kuwafikia Watanzania wengi.
Alisema huduma hiyo itasaidia kuweka na kutoa fedha kwenye
akaunti za wateja wa CRDB, kutuma fedha kwa watu wenye akaunti na wasio na
akaunti za benki, kupokea fedha walizotumiwa na wateja, kupokea marejesho ya
mikopo mbalimbali, kulipia Ankara, kuangalia salio na kuhamisha fedha kwenda
kwenye akaunti nyingine ndani ya CRDB.
Dk. Kimei alisema ingawa huduma ya fahari kupata mafanikio
kwa kipindi kifupi bado Watanzania wengi wako nje ya mfumo huo na kueleza
kwamba ni asilimia 17 ya watanzania wote walio kwenye mfumo halali wa fedha.
Alisema kwamba kwasasa wana mawakala 1,500 wameshajiunga na
kuanza kutoa huduma kwa wateja ambapo wastani wa miamala 300,000 hufanyika kila
mwezi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Tanzania, Juma Rajabu,
alisema ni fahari kwa kampuni yao kupata fursa ya kufanya kazi na CRDB na
kuahidi kuendelea kujiimarisha ili kuweza kuwafikia Watanzania wengi.
Post a Comment