PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAJAMBAZI WAVAMIA KITUO CHA POLISI STAKISHARI UKONGA JIJINI DSM NA KUUA ASKARI KISHA KUPORA SILAHA USIKU WA KUAMKIA LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
IGP MANGU akizungumza na waandishi wa habari mapema leo juu ya uvamizi huo uliofanyika katika kituo cha polisi staki shari ukonga jijini D...
IGP MANGU akizungumza na waandishi wa habari mapema leo juu ya uvamizi huo uliofanyika katika kituo cha polisi staki shari ukonga jijini DSM na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano  kwa polisi ili waweze kuwakamata wahalifu waliotenda kitendo hicho
mmoja wa wa mmama aliyeuwawa katika tukio hilo

polisi aliyeuwawa na majambazi

mmoja wa raia aliyeuwawa katika tukio hilo
WATU walio na silaha za moto wamekivamia kituo cha Polisi Staki Shari Ukonga na kuwaua watu 7 wakiwepo Polisi wanne.

Taarifa kutoka eneo hilo la tukio ambapo Kituo hicho ni Makao Makuu ya Polisi Wilaya ya Ukonga zuinaarifu kuwa watu hao ambao idadi yao haijajulikana walivamia majira ya saa tano usiku wa Julai 12 mwaka huu.

Mbali na kuuwa watu pia inadaiwa kuiba silaha kadhaa kituoni hapo zikiwepo SMG 15 na SR 6 na risasi.

Mmoja wa watu waliouwawa katika tukio hilo inaelezwa kuwa ni dereva wa bodaboda aliyetambulika kwa jina maarufu Mandevu ambaye inaelezwa alikuwa amewapeleka watu hao kituoni hapo  lakini wakati wa kuondoka pikipiki yake iligoma kuwaka na hivyo kupigwa risasi na wahalifu hao.
Tunatoa pole kwa Jeshi la Polisi Tanzania na familia za wote waliofikwa na msiba huo huku tukiomba jamii kutoa taarifa za haraka juu ya wahalifu hao kwani silaha hizo zitatumika katika matukio ya kihalifu na kuleta athari klwa jamii.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top