Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Waziri wa
Habari,utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk pamoja na washabiki wa
Tamasha wakimshangiria Kiongozi wa Ngoma ya Utamaduni ya Lelemama akifanya vitu
vyake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanibari.
Vazi lenye asili ya watu wa Kitumbatu walilokuwa wakilitumia wakati
wakielekea mashambani huku mwana Mama anatembea akisuka ukili kuashiria ufundi
wa utamaduni wa asili.
Muimbaji mahiri wa Visiwa vya Comoro al anisa Shamsia Sagaf akitumbuiza
kwenye uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibari hao Bwawani Mjini
Zanzibar.
Kikundi cha akina mama watupu wakitumbuiza ngoma ya asili ya Lelemama
kwenye uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibari Mgeni rasmi alikuwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AlI Iddi kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Hilo ni onyesho la asili la Koti, kanzu na kofia kwa mwanamme na
Bui Bui la Kamba lililokuwa likivaliwa na akina mama wa zamani.
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein
amewakumbusha Wananchi wote Nchini kuelewa kwamba heshima na tabia njema
iliyojengeka katika nyoyo za Watu wa Zanzibar kutokana na kupenda, amani na utulivu ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Wazanzibar.
Alisema ni
muhimu kwa kila Mwananchi kuhakikisha anatoa mchango wake katika kulinda,
kuukuza na kuutangaza utamaduni wa Mzanzibari kwa kuzingatia mambo mazuri
wanayoyapenda wananchi wenyewe.
Dr. Ali
Mohammed Shein alitoa kauli hiyo wakati
akilizindua Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibari katika Hotuba iliyosomwa
kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo
katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Alisema endapo
mkakati wa makusudi utawekwa wa kuwashawishi wageni kuiga mambo ya asili na
utamaduni wanaoutembelea bila shaka wageni na watalii hao watavutiwa na
kuyapenda na hatimae masuala hayo yatalipatia sifa Taifa hili.
Rais wa
Zanzibar Alisema kwamba Zanzibar ina Historia inayowavutia wageni mbali mbali
kutokana na Utamaduni wenye mchanganyiko wa mambo mengi jambo ambalo limevipatia
heshima ya pekee Visiwa vya Zanzibar.
Alisisitiza
jukumu la kila Mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuvikataa na kuvipinga
vitendo vinavyotia doa,Desturi, mila na Utamaduni ikiwa ni pamoja na vitendo
vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo hivi sasa Serikali inaendelea na juhudi
mbali mbali za kuvikomesha.
Aidha alitoa
wito kwa Wananchi waendelee kuunga mkono kampeni inayofanywa na Serikali Kuu
dhidi ya unyanyasaji wa Kijinsia iliyoianzisha Tarehe 6 Disemba mwaka 2014
isemayo Zanzibar bila ya udhalilishaji wa kijinsia inawezekana.
Ujumbe wa
Mwaka huu wa Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibar “ Tudumishe Utamaduni wetu
katika hali ya amani, utulivu na Umoja".
Post a Comment