PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DK. BILALI AFUNGUA MAONESHO YA KUMI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VIKUU NCHINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua   rasmi Maonesho ...

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akioneshwa Plastiki zilizotengenezwa  kwa kutumia Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha The United African University Of Tanzania (UAUT) Chang Kilee, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya  Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja kati ya mashine za kufanya miamala za Max Malipo, huku akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Machungu Msama,  wakati alipotembelea banda lao la maonesho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top