PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Wabunge wafurahia muswada wa kuiboresha benki ya posta Tanzania
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  BAADHI ya wabunge wamesema kuwa muswada wa sheria kufuta sheria iliyoanzisha benki ya Posta na kuifanya ijiendeshe kibiashara, ume...

 Wabunge wafurahia muswada wa kuiboresha benki ya posta

BAADHI ya wabunge wamesema kuwa muswada wa sheria kufuta sheria iliyoanzisha benki ya Posta na kuifanya ijiendeshe kibiashara, umekuja kwa wakati na utaondoa malalamiko ya benki nyingine dhidi ya serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula, akizungumza wakati wa semina ya wabunge juu ya muswada wa sheria ya benki ya posta, muswada wa sheria ya matumizi ya mapato ya gesi na muswada wa sheria ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa.
Alisema benki ya posta inajiendesha kwa sheria ya zamani, na kwa sheria mpya itaondoa malalamiko ya benki nyingine kuwa inafanya makosa lakini yanafumbiwa macho na serikali, hivyo ni vyema isajikiwe kibiashara na hivyo kuepusha bunge kuwa sehemu ya kuvunja sheria.
Awali, Mkurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi, alisema wananchi wanapaswa kuelewa kuwa muswada huo hauji kuifuta benki hiyo balk kuboresha utendaji wake kwa kuwa ya kibiashara na kuwa benki kubwa Tanzania.
Serikali inamiliki hisa asilimia 86 ndani ya benki hiyo, Posta na simu asilimia nane na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar asilimka tatu, na kwamba huduma za kibenki kwa simu ni zaidi ya 250,000.
Naibu Katibu Mkuu Wiraza ya Fedha, Adolf Mkenda, alisema  muswada hup ni mzuri kwa kuwa italiwezesha taifa kupiga hatua kimaendeleo, lakini wananchi wanapaswa kuelimishwa kuwa lazima sekta nyingine ziendelee ili kueousha nchi kukubwa na ugonjwa wa kutegemea kitegauchumi kimoja na kuua sekta nyingine.
"Kuna changamoto mbalimbali kama kutegemea gesi pekee bali tuweze kupiga hatua kwa kuwa na uwekezaji mkubwa kama kutengeneza simu,,gesi iliyopo inaisha mwaka 2051, hivyo sekta zote zinapaswa kukua kwa pamoja na gesi," alisema.


Mkenda alisema changamoto nyingine ni ufisadi kwa baadhi ya watu kutumia vibaya fedha hizo ndiyo maana serikali imeleta sheria ambayo itakuwa na masharti magumj ya kubadilisha.
Wakichangia miswada hiyo, Mbunge wa Ngara ( CCM), Deogratus Mtukamazima, alisema sheria na miongozo mizuri iliyopo itategemea serikali itakayokuwepo madarakani ambayo itakuwa na utawala bira na isiyosimamia misingi ya ryshwa.
"Tukiwa na serikali dhaifu na inayoendekeza rushwa tutaishia kuwa kama Nigeria, tunahitaji serikali imara kusimamia sekta hii, wapo baadhi ya wawekezaji ni matapeli , pia wanasheria na wataalamu lazima waiangalie kwa kina mikataba inayoingiwa, lazima tuwadhibiti wawekezaji mataoeli na hilo litawezekana kwa kuwa strong goverment," alifafanua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalum, Prof. Mark Mwandosya, alisema kupitishwa kwa miswada hiyo ni kuandima historia kwa taifa na kwamba wanasiasa na viongozi wanapaswa kuelimisha umma kutokuwa na matarajio makubwa katika sekta moja kwani gesi siyo mwarobaini na isiwe chanzo cha matatizo nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top