PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA MFUMO WA BVR WAGEUKA BIASHARA JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kinamama wakifanyabiashara ya mama ntilie katika kituo cha kupiga kura cha kata ya Sombetini jana ,vituo vya kujiandikisha vinakabiliwa...
Kinamama wakifanyabiashara ya mama ntilie katika kituo cha kupiga kura cha kata ya Sombetini jana ,vituo vya kujiandikisha vinakabiliwa na idadi kubwa ya watu hali inayopelekea foleni ndefu na watu kukesha kwenye vituo.Picha na Ferdinand Shayo



Wakazi wa kata ya Sinoni wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kupiga kura,vituo vinakabiliwa na idadi kubwa ya watu ukilinganisha na uchache wa  mashine za BVR .Picha na Ferdinand Shayo






Na Ferdinand Shayo,Arusha.



Zoezi la Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  kwa mfumo wa kisasa wa BVR umechukua sura mpya kutokana na baadhi ya watu  kuwauzia watu nafasi za kuingia katika vituo vya kujiandikishia hivyo  kugeuka biashara  kwa wanaokwepa foleni ndefu na kukesha katika vituo.



Wananchi wa Kata ya Sinoni jijini hapa  Hussein Issa na Swalehe Ramadhani wameeleza kuwepo kwa baadhi ya vijana ambao wamekwisha kujiandikisha lakini hufika kituoni hapo na kushika nafasi za mbele ambazo wanawauzia watu wengine mchezo ambao umekithiri katika vituo vingi.



Issa alisema kuwa nafasi moja huuzwa kati ya shilingi 15000 hadi 10000 kwa mtu mmoja  nafasi hizo hugombaniwa na watu wengi  .



“Watu  wamegeuza BVR kama biashara wanashika nafasi na kuwauzia watu jambo ambalo linakwamisha zoezi wengi wasiokuwa na kitu cha kutoa wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu bila mafanikio” Alisema Issa



Polpodia Massawe mkazi wa Esso analalamikia mfumo huo kuwa bado haujaweza kukidhi idadi kubwa ya watu kwani imemlazimu kuacha shughuli za kujiingizia kipato na kupanga foleni kwa muda wa siku 4 bila mafanikio.



Aliasema kuwa watu wengine wamekua wakikesha na kulala vituoni hapo ili kuwahi nafasi hadi kinamama wenye watoto wadogo hivyo ameitaka serikali iongeze nguvu hasa kwenye vituo vya mijini vyenye idadi kubwa ya watu.



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Filex Ntibenda aliyetembelea kituo hicho amekaripia vikali tabia ya watu kuuza nafasi maarufu kama ploti kwani ni kinyume cha utaratibu pia amewataka wanasiasa kutoingilia suala la uandikishaji na kuishia kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi.




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top