
KATIKA jitihada za kuwafikia Watanzania mbalimbali Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua akaunti maalum kwa ajili ya Vikundi Visivyo Rasmi. Uzinduzi huo ulifanywa na Katibu Mtendaji wa Shirika la Uwezeshaji Tanzania, Beng’I Issa katika viwanja vya Shule ya Msingi Osterbay, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema, sasa makundi mbalimbali yasiyo rasmi yanaweza kufungua akaunti na Benki ya Posta na kuweza kupatiwa mikopo ya riba nafuu ya kuwawezesha katisha shughuli zao za ujasiriamali.
Makundi mengi yamejitokeza katika kufungua akaunti hizi za vikundi visivyo rasmi, na hadi sasa akaunti takribani 340 zimefungulia kwa makundi yasiyo rasmi, alisema Moshingi. Kwa wiki benki inafungua akaunti zaidi ya 16 kwa makundi haya, na tunapenda kuwahamasisha makundi haya yajitokeze kwa wingi, ili waweze kunufaika na akaunti hii, alisema Moshingi.
Kwa upande wake Beng’i Issa, alitoa pongezi kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kubuni akaunti hiyo maalum kwa makundi hayo. ‘Makundi mengi yanatamani sana, kupata huduma za kibenki kwa ajili ya shughuli zao za kila siku, ila kutokana na uwezo sababu zilizo nje ya uwezo wao wanashindwa kupata huduma hizo’, alisema Issa. Sasa makundi haya yajitokeze kwa wingi katika kufungua akaunti hii Benki ya Posta iliwaweze kupata huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo, mikopo n.k aliongeza Issa.
Benki ya Posta Tanzania ni miongoni mwa mabenki yanayokuwa kwa kasi nchini, ikifuata sera ya financial inclusion, yaani kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za kifedha hapa nchini.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.