Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola
Foundation ,Elisha Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watoto wa mitaani walioko jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo
maalumu vya malezi lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa
ya elimu waliyoikosa kwa muda mrefu.
Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu
ambapo mpaka sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha
malezi kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa na
kuchukuliwa na wazazi wao.
Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda
mrefu hujitumbukiza katika majanga ya matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya
vitendo visivyofaa hivyo ameitaka jamii ishirikiane kutatua tatizo hili ambalo
ni janga kwa taifa.
“Tunapofika mtaani kuwaondoa watoto hawa wa mtaani
tunakutana na changamoto nyingi ikiwemo kukosa ushirikiano na watoto wenyewe na
pia wengine wanatumkishwa na ajira katika umri mdogo na baadhi ya watu hivyo
kufanya zoezi hilo kuwa gumu” Alisha Elisha
Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini A
Mwantumu Dossi alifika katika kituo cha
kufikia cha malezi ya watoto wa mtaani kinachomilikiwa na Gola Foundation amesema
kuwa Halmashauri ya jiji itaangalia namna ya kushirikiana kutatua changamoto za
watoto wa mitaani.
“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu nimefika apa
kujionea na kama Jiji kuna mkakati Mahususi wa kuwaondoa watoto wa mitaani
utakaoanza 2015-2016” alisema Mwantumu
Mwenyekiti wa Baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassan Omari
alisema kuwa juhudi za kuwaondoa watoto wa mitaani katika mazingira magumu na
hatarishi zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu pamoja na serikali kwani watoto
ni taifa linalotegemewa kesho.
Post a Comment