Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Askofu Mkuu wa Kanisa la
International Evangelism Church Eliud Isanja amewataka Watanzania
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutimiza
haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo ya
taifa.
Isanja aliwaasa Watanzania
kutozembea nafasi hiyo muhimu na badala yake waitumie fursa hiyo
itakayoleta mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.
Akizungumza katika mahafali ya
Wahitimu wa Diploma ya masomo ya Biblia amesema kuwa Tanzania inahitaji
Viongozi waadilifu na wenye bidii.
“Watu wasipige tu kelele barabarani
bali wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi bora
watakaoliongoza taifa hili” Alisema Isanja
Kwa upande wake Askofu Mwangalizi
wa Kanisa hilo Israel Maasa ambaye alikua mgeni wa heshima katika
mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa
misingi ya ukabila na udini na kutowachagua kwani wataathiri umoja na
mshikamano wa kitaifa.
Wilfred Pallangyo ameeleza kuwa ni
wakati wa Watanzania kuwatambua viongozi watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa
nafasi hiyo pasipokufanya makosa pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa
tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa Tayari zoezi la uandikishaji limeanza katika
baadhi ya mikoa na linategemewa kukamilika nchini kote ili kukamilisha
uchaguzi utakaoanza Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza
tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.
Post a Comment