Pichani
juu na chini ni Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za
utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo
mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda
la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii
Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za
vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika
ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.
Afisa
Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon
(kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical
Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na
Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania
kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio
vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi
jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.
Wageni
mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania
wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa
mbalimbali kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la
Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es
Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe
kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.
Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris
nchini Tanzania, Mary Joel akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za
utalii zinazofanywa na kampuni yake kwa wageni waliofika katika banda la
Tanzania wakati wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (wa pili kulia)
akitoa maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za
vivutio vya utalii nchini Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la
Tanzania kwenye maonyesho nane ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World
Tourism Expo) jijini Harare.
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel
ya nchini Tanzania, Joseph Waryoba (kulia) akipata picha ya kumbukumbu
na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Zambia, Felix Chaila
aliyembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya siku tatu ya utalii
ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli
ya Rainbow Towers ambayo yamemalizika juzi.
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel
nchini Tanzania, Joseph Waryoba katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah ambaye pia ni Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Tanzania Travel Company ambayo pia imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
Timu kutoka Tanzania ambayo imeshiriki maonyesho
ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini
Harare ikiongozwa na Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB), Esther Solomon (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Wakala wa
utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba, Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (kulia).
TIMU
ya watanzania walioenda kuhudhuria maonesho ya utalii nchini Zimbabwe
wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza uendeshaji wa sekta ya
utalii.
Walisema
katika ziara yao hiyo wamegundua kwamba Wazimbabwe kuanzia wanapompokea
mgeni hadi anapofika hotelini wanaonesha kujali hali ambayo mgeni
hawezi kusahau hata kidogo.
Aidha amesema kwamba hata mipangilio ya kwenda kwenye vivutio inafanyika katika hali ambayo huwezi kusahau hata kidogo.
Kutokana
na mazingira hayo, wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza
namna ya kupokea na kuishi na wageni na kuwatengenezea taswira ambayo
hawatakaa wakisahau.
Hayo
yamesemwa na Ofisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),
Esther Solomon katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog
yaliyofanyika mjini Harare siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya siku
tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare
katika hoteli ya Rainbow Towers jijini Harare.
Solomon
amesema ingawa hali ya Tanzania si mbaya, watendaji katika viwanja vya
ndege na mahotelini wanaweza kuangalia namna Wazimbabwe wanavyojali kazi
zao na tabasamu zao nyakati zote kwa wageni .
“Si
kwamba kwetu kuna shida lakini unaona watu wanavyojituma hapa” alisema
Esther Solomon na kuongeza kuwa aliona jinsi walivyojipanga vizuri na
wafanyakazi walikuwa na uelewa wa hali ya juu.
Esther
aliongoza kundi la watu watano wa Kitanzania walioalikwa na mamlaka ya
utalii Zimbabwe (ZTA) kuhudhuria maonesho hayo.Tanzania iliweka banda
lake pia katika maonesho hayo ya siku tatu yaliyomalizika juzi.
Makampuni ya mawakala wa utalii aliyoambatana nayo katika safari hiyo ni pamoja na Tanzania Travel Company, Cordial Tours and Travel, Mberesero Tented Camp na Best Northern Tours and safaris .
Alisema
safari yao Zimbabwe pamoja na ushiriki wao katika maonesho pia walifika
katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini yakiwemo maporomoko ya
Victoria.
Aidha walipewa nafasi ya kukagua sehemu za malazi kwa ajili ya wageni.
Alisema
katika maonesho hayo wamefanikiwa kupata wageni wengi wanaoulizia namna
ya kufika Tanzania na pia ushirikiano wa makampuni katika sekta ya
utalii.
“
Watu wengi wamekuja kututembelea. Na wengi ni watu weusi. Mwamko wao wa
kutembelea vivutio ni mkubwa.” Alisema Esther na kuongeza kuwa wamebaini
kwamba ipo haja ya watanzania kuhimizwa kutembelea vivutio kwani hata
nchini Zimbabwe wanaotembelea vivutio ni wananchi wenyewe.
Alisema wengi waliofika katika banda la Tanzania waliulizia namna ya kufika visiwa vya Zanzibar na pia mbuga za Tanzania.
Aidha mawakala wengi waliulizia namna ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utalii katika bara la Afrika.
Asilimia 80 ya watalii nchini Zimbabwe wanatoka bara la Afrika na waliobaki ndio wanatoka nje ya bara hili.
Post a Comment