PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAFUGAJI WATAKIWA KUFUGA KISASA ILI KUKUZA UCHUMI WAO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wanachama wa ushirika vya Wafugaji vya Leo Pastoralist kilichopo wilaya ya Longido mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Viong...
Wanachama wa ushirika vya Wafugaji vya Leo Pastoralist kilichopo wilaya ya Longido mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa mashirika binafsi ikiwemo African Wild life Foundation (AWF).Picha na Ferdinand Shayo


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wafugaji  wa Vijiji vya Enduimet na Tinga tinga  vilivyopo wilaya ya Longido mkoani Arusha wametakiwa kufuga kisasa ili waweze kuvuna mazao bora ya maziwa na nyama ambayo watayauza na kukuza  uchumi wao badala ya kujivunia kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija kiuchumi.

Akizungumza na Wafugaji wao kutoka vyama vya ushirika vya Wafugaji vya Leo Pastoralist Cooperation pamoja na Tinga Tinga pastoralist cooperation ,Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la uhifadhi wa Mazingira na viumbe hai la African Wild life Foundation (AWF) upande wa Hifadhi ya milima Kilimanjaro ,Noah Sitati amesema kuwa licha ya  kupata manufaa ya kiuchumi wanayoyapata wafugaji hao pia wanapaswa kuwasomesha watoto wao ili kuchochea maendeleo kwa jamii ya Wafugaji.
Sitati amesema kuwa wako kwenye mpango wa kuwasaidia wafugaji hao kupata madume ya kisasa yatakayowawezesha kupata mbegu bora za ng`ombe wa maziwa na nyama hivyo kukuza uchumi wao.

“Ufugaji wa kisasa unaleta manufaa makubwa hata ukiwa na mifugo michache ambayo utaitunza vizuri tofauti na kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambayo hawasaidii kuinuka kiuchumi” Alisema Sitati


Kwa upande wao Wafugaji kutoka vyama hivyo vinavyofadhiliwa na AWF  wameeleza kuwa vyama hivyo Hamisi Hassani na Isack Ole Ndereko wamesema kuwa vyama  hivyo vya usharika vinawasaidia kuwa na sauti moja na kupiga hatua kiuchumi kupitia misaada ya kitaalamu pamoja na fedha ambazo wanaziweka akiba na kukopeshana ili kukuza uchumi wa wafugaji.


Afisa Programu  wa  Shirika la kimataifa la uhifadhi wa maliasili International Union for Consevation  of nature  (IUCN)  lenye makao yake nchini  Kenya,Akshay Vishwanath   amesema kuwa umoja wa wafugaji utawasaidia kukuza shughuli zao na ustawi katika kujiletea maendeleo .



Licha ya Tanzania kuwa moja kati ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na idadi ya mifugo bado sekta ya ufugaji nchini haijachangia kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wingi wa mifugo,changamoto ambayo ikitatuliwa huenda sekta ya ufugaji ikakuza uchumi na kuondoa umasikin

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top