Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Taasisi
isiyo ya kiserikali inayojihusisha na watoto wanaoishi katika mazingira magumu jijini
Arusha Gola Foundation imeanzisha kitengo cha kuwasaidia watoto na vijana ambao
ni waathirika wa madawa ya kulevya ili wapate matibabu na kuachana na matumizi
ya dawa hizo na kuweza kushiriki vyema katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Mkurugenzi
wa Shirika hilo Elisha Maghembe amesema kuwa kwasasa wanacho kituo cha watoto
na vijana 25 wa mitaani ambao wameanza kupatiwa matibabu kituo ambacho kipo
mbali na mji ili kuwatenga watoto hao na mazingira hatarishi ambayo huwashishi
kurudi katika hali zao za awali.
Maghembe
alisema kuwa katika kituo hicho vijana hao wanajishughulisha na shughuli za
kilimo shughuli ambayo inawaingizia kipato hivyo kuwaepusha na vitendo vya
uporaji na biashara haramu.
Hivyo
ameiomba jamii kuungana pamoja kuwasaidia watoto wa mitaani ,wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na
waathirika wa madawa ya kulevya na
kuokoa vijana wenye nguvu,vipaji na uwezo mkubwa unaoteketea kwa madawa badala
ya kuwa rasilimali ya taifa.
Daktari wa
Shirika la Wamisionari (Medical
Missionaries lifestyle center for East Afrika) Kefa Omari ambaye alifika katika kituo hicho jana
na kutoa msaada wa kitabibu kwa vijana
hao pamoja na madawa ya kuondoa sumu inayotokana na madawa hayo katika mwili.
Kefa ameshauri vijana hao kuzingatia kanuni bora za afya ikiwemo
kupata lishe bora,kuzingatia mazoezi,unywaji maji,kutenga muda kupumzika kwasababu inawezekana kuachana kabisa na
matumizi ya madawa hao na kurudi katika hali ya kawaida.
Kenedy
Njenga na Francis Oni ni Vijana wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Arumeru wamesema kuwa kwasasa wameamua kuachana na
madawa ya kulevya kwa kipindi kirefu wamekua wakiathirika kiafya na kiuchumi
hivyo wanatumia nafasi hiyo kufanya
shughuli za kijamii kama kilimo pamoja na kujitolea .
Post a Comment