PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ZAIDI YA EKARI 300 ZA MAHINDI ZAHARIBIOWA NA WAFUGAJI WILAYANI KIOTETO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
EKARI 300 za mazao ya mahindi kwenye eneo la Kaa Chini, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, zimeharibiwa baada ya kuliwa na mifugo kutok...



EKARI 300 za mazao ya mahindi kwenye eneo la Kaa Chini, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, zimeharibiwa baada ya kuliwa na mifugo kutokana na migogoro na mvutano baina ya jamii ya wafugaji na wakulima wa sehemu hiyo.
Hata hivyo, wakulima wa eneo hilo Abasi Ally na John Peter, wameiomba serikali kutoa tamko kutokana na tukio hilo la mazao yao kuteketezwa baada ya baadhi ya wafugaji wa Kaa Chini kuchungia mifugo katika mashamba yao.
Peter alisema wafugaji hao walifanya tukio hilo la kinyama juzi kwa kuingiza mifugo kwenye mashamba yao na kuwapa hofu ya kutokuwa na chakula pindi msimu wa mavuno utakapofika na hatambui nani atakayefidia hasara yao.
Akizungumzia kuhusu hilo, diwani wa kata ya Njoro Iliasa Saidi alisema wafugaji hao walichungia mifugo kwenye mazao yaliyokuwa katika eneo hilo, baada ya kudai kuwa wakulima walilima mashamba sehemu ya hifadhi ya jamii (WMA).
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Kiperesa Mustapha Omary alisema imekuwa ni jambo la kawaida kwa wakulima kulishiwa mashamba yao na jamii ya wafugaji, bila hatua yeyote kuchukuliwa na serikali.
“Hili suala linatakiwa kuchukuliwa hatua kwani mapigano ya wakulima na wafugaji husababishwa na vitu kama hivi japokuwa tuliwasihi wakulima wasichukuwe sheria mkononi ndiyo hali ya amani ikawepo,” alisema Omary.
Mwanzoni mwa mwaka huu, zaidi ya wakulima 20 walikamatwa shambani na matrekta yao, wakidaiwa kuvamia na kulima mazao kwenye hifadhi ya jamii WMA, iliyopo kwenye vijiji vya Makami, Ndego, Ngabolo na Katikati.

CREDIT: SAUTI YA MNYONGE

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top