WAFANYABIASHARA
wadogo wa Madini aina ya tanzanite na madini mengine wanaofanya
shughuli zao Mtaa wa Pangani jijini hapa wamemuomba Rais Jakaya Kikwete
kumbakiza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele katika
nafasi aliyonayo kwani anajali matatizo ya wachimbaji wadogo.
Aidha
wamesema endapo Masele akiondolewa katika nafasi hiyo ndoto yao ya kuwa
na jengo la kisasa la uuzwaji wa madini hayo litakalojulikana kwa jina
la Tanzanite Complex zitakufa.
Walieleza
kuwa kwa miaka mingi mawaziri na naibu mawaziri waliohudumu katika
Wizara ya Nishati na Madini hawakuwa na ndoto ya kujenga jengo hilo
litakalowawezesha wafanyabiashara kuuza madini hayo jijini Arusha.
Wakizungumza
jana jijini hapa wafanyabiashara hao walisema wanamuomba Rais Kikwete
kumuona Masele kuwa hana hatia na ni kijana mdogo anayefaa kuongoza
katika sekta hiyo kwani wachimbaji madini na wafanyabiashara wa madini
karibu nchi nzima wanamkubali kwa sababu ya kujali matatizo yao.
Mfanyabiashara
wa tanzanite, Godfrey Silvester akizungumza kwa niaba ya wenzake
alisema tangu Masele alipochaguliwa kuwa Naibu Waziri ameweza kukutana
na wachimbaji wadogo kutatua changamoto zinazowakabili.
Pia
amewasaidia kutoa fursa za ukopaji wa mikopo kupitia Benki ya
Rasilimali (TIB) ili kuwawezesha kupata vifaa vitakavyowarahisishia
kuchimba madini hayo kisasa zaidi.
â€Å“Tunamuomba
Rais Kikwete asimtoe Masele katika wadhifa wake kwani ni mtetezi mkubwa
kwetu sisi wafanyabiashara na wachimbaji wadogo wa madini ametuonesha
njia mbalimbali za kufanya biashara zetu kuwa za kisasa,†alisema
Silvester.
Post a Comment