PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: VETA WATAKIWA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU ILI KUJUA MAHITAJI YAO SANJARI NA KUBADILISHA MITAALA YA ELIMU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamanolililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya k...



WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamanolililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao




waziri wa ajira na kazi Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau waliouthuria katika konga mano hilo

Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Bg Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni mkurugenzi wa VSO Tanzania

picha ya pamoja ya washiriki wa kongamono hilo wakiwa pamoja na waziri wa ajira na kazi nje ya ukumbi wa hotel ya Naura Springs iliopo ndani ya jiji la Arusha

waziri kabaka wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi ayupo pichani kuhusiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)
WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano
baadhi ya waandishi wakiendelea kufatilia kwa makini kongamano hilo
washiriki wakifuatilia


picha wakwanza kulia ni mwenyekiti wa bodi ya veta Idrissa Mshoro wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi wakiwa wanamsikiliza waziri hayupo pichani








washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini




Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akiwa anaongea katika kongamano hilo
wadau kutoka sekta ya gesi na petrol wakiwa wanafatilia
katibu mkuu wa VET Pro.Sifuni Mchome akiwa anawakilisha mada


Na Woinde Shizza,Arusha
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo hivi sasa.

Hayo yanesemwa leo jijini hapa na WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana

Aidha aliwataka vijana kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze kujiariri badala ya kufanya biashara za kuuza vitu mikononi bali watumie taaluma walizozipata kuzalisha vitu vyenye ubora.

Alisema vijana wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya uhakika.


waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji mwenyekiti wa bodi

Alisema ni vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wan chi.

“Mahitaji ya vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta inamtegemea mtu fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau sambamba na kutafuta mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji ya soko na nyinyi vijana tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi ili kuweza kuuza biashara zenu kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza barabarani “.

Naye Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo hufanyika kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili kujadili masuala mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya ajira sambamba na kuboresha mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha vijana wanaopitia Veta kuwa bora zaidi kipindi cha kumaliza chuo na kupata ajira.

Alisema pia Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha kwenye ujenzi wa vyuo vipya kwenye Wilaya mpya ambazo ni Katavi, Geita, Njombe na Simiu lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali ambao wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali yanayowawezesha kupata ajira.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa Veta inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira ndio maana vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa makini na kujipatia vipato zaidi.


Aliongeza kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali hususan ya sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya kuwasaidia vijana kukabiliana na soko la ajira .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top