RAISI KIKWETE APANGUA SAFU YA WAKUU WA MIKOA TENA, MBWILO APELEKWA PWANI MKUU WA WILAYA YA KARATU AULA......
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja
wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi
wengine sita kuanzia jana, Jumamosi,
Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili,
Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu
Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue
mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais
amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu,
Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix
Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho,
Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne
asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.
Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu
waliohamishwa vituo vya kazi ni
Mheshimiwa Elaston Mbwilo
anayehamishwa kutoka Mkoa wa
Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu
ambako anachukua nafasi ya
Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa
likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel
Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa
wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro
na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M
Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa
Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi
Magalula anayehamishiwa Mkoa wa
Tanga kutoka Mkoa wa Lindi,
Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza
anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka
Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa
Mhandisi Evarist B. Ndiliko
anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka
Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa mikoa
wanaendelea kubakia katika vituo
vyao vya sasa vya kazi
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam
6 Desemba, 2014
Post a Comment