Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Maisha ya mtu ni
matunda ya mtiririko wa maamuzi ya mtu binafsi yakiwa yamechanganyika na
maamuzi ya watu wengine yanayogusa maisha yake.
Maisha uliyonayo ni matokeo ya maamuzi uliyoyafanya,nyumba
uliyonayo,elimu uliyonayo,mke au mme,uchumi,biashara unayoifanya.
Uko hivyo ulivyo kutokana na maamuzi uliyoyafanya na unayoendelea
kufanya ,maamuzi ya leo ni matokeo ya kesho amua vyema upate vyema.
Mafanikio yako ya kesho yanategemea maamuzi unayoyafanya leo hivyo uamuzi unaoufanya una nguvu ya
kubadilisha maisha yako.
Hakuna mtu anaweza kubadilisha maisha yako isipokuwa wewe na
maamuzi yako amua kubadilika amua kufanya maamuzi sahihi upate kuishi maisha
sahihi.
Kabla ya kufanya uamuzi fikiria matokeo ya maamuzi kwa
mantiki hii jambo linalofanyiwa maamuzi si la kufanyiwa mzaa wala uzembe.
Watu wengi hawafanikiwi katika maisha yao kwasababu si
waangalifu juu ya maamuzi
wanayoyafanya.Usifanye maamuzi ambayo yanamfurahisha mtu lakini baadae
yanakusababishia majuto na uchungu.
Maamuzi yanakusaidia kufika pale unapotaka kufika ,maisha
yetu ni matokeo ya maamuzi yetu .Maisha ya baade yanategemea maamuzi
tunayoyafanya leo.
Kufanikiwa ni uchaguzi na kutofanikiwa pia ni
uchaguzi,maisha ya mtu yanaendesha na maamuzi ama uchaguzi na si majaliwa wala
bahati nasibu wala bahati mbaya,kama zipo ni nadra sana ila zaidi ya asilimia
90% ya maisha yetu yanatokana na maamuzi yetu.
Maamuzi unayoyafanya
yanaweza kwenda kwa watoto,wajukuu na vitukuu, vizazi na vizazi vijavyo
vinaweza kunufaika na maamuzi yako ama kuathiriwa kwa maana ya kupata madhara.
Kila siku binadamu anafanya maamuzi ,hivyo maamuzi ni kitu
ambacho hakiepukiki ,hakikwepeki ,maisha yanatuweka njia panda mara kwa mara na
kututaka tuchague.
Watu wengi wanakosa utulivu wa ndani wa kufanya maamuzi
wanajikuta wanafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kuishi maisha ambayo si
sahihi.
Maamuzi yako yanaweza kubadilisha mustakabali wa maisha yako
,hivyo usiuchekee uamuzi utakaokupa majuto baadae,utakao kubakiza kwenye
umasikini na matatizo uliyonayo.
Maaumuzi ni gharama ya kulipia maisha,kama kuna mambo
unayahitaji kwenye maisha yako yanaweza kubakia kua ndoto au kwenye mawazo
mapaka utakapoamua kuyatoa kwenye uhalisia na kujimilikisha.
Fanya maamuzi sahihi uapate maisha sahihi.
0765938008
Post a Comment