Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Ni Ukweli
usiopingika kuwa maisha tuliyonayo
yamejaa ushindani,hivyo ushindani hauepukiki tunakutana nao kwenye kila kona ya
maisha iwe ni uchumi,kazi,siasa,mahusiano.
Katika
mashindano kuna matokeo ya aina mbili pekee kushinda na kushindwa hakuna droo
kwenye maisha.
Kwa mantiki
hiyo kama maisha ni ushindani tunapaswa kujiandaa si tu kujiandaa kushindana
bali kujiandaa kushindana na kushinda.
Maisha
yanafanana na mashindano ya kupiga mbio kwa lugha ya kigeni wanaita Marathon
ambapo wapiga mbio ni wengi lakini washindi ni wachache.
Maandalizi
ni muhimu kama tunahitaji kushinda kwenye kila jambo elimu,biashara .Mara nyingi
mashindano hayana miujiza kushinda na kushindwa kunategemea na jinsi
ulivyojiandaa.
Wahenga
waliwahi kusema kuwa maisha fainali uzeeni .Unapofika umri Fulani unaanza
kufaidi matunda ya juhudi zako ,kama hukuweka juhudi inakua tofauti,kupata ushindi kunatokana na
nguvu ya maandalizi.
“Usipojiandaa kushinda jiandae
kushindwa” Anaeleza
Msanii Fareed Kubanda katika wimbo wake wa siri ya mchezo akieleza umuhimu wa
maandalizi.
Maisha yanahitaji
mpangilio,mipango thabiti,mikakati na utekelezaji ambao ndio maandalizi ya
kushinda katika maisha.
Watu wengi wanajiandaa kushindana
lakini sio kushinda wanajikuta wamekua washiriki wa mashindano lakini sio
washindi,Muhimu ni kujiandaa kushindana na kushinda.
Unapojiandaa
kushindana na kushinda unatengeneza stamina ,ustahimilivu na uvumilivu wa
kutosha ndani yako.
Haijalishi
magumu unayoyapitia ,maumivu unayoyapata ,macho yako yatakua yanatazama
kuelekea ushindi ulipo kuliko kutazama magumu na maumivu hivyo utajikuta ukikaza mwendo kuyaelekea
mafaniko ama ushindi.
Ukijiandaa
kushindana na kushinda unatengeneza shabaha ndani yako kwani mara zote unauona
ushindi ndani yako na nje.
Maandalizi
yanatengeneza picha ya ushindi katika
moyo wako ,akili yako na si picha ya mashindano.
Unapoenda
kushindana kichwani kwako una picha ya mashindano na si ya ushindi unaweza
kuishia kuwa mshiriki wa mashindano na si mshindi.
Kujiandaa
kushindana na kushinda kunatengeneza kiu ya kufikia ushindi ,tama,shauku ya
kushinda hilo linatengeneza msukumo wa
ndani wa kuufikia ushindi ,msukumo ambao unazaa msukumo wa nje ambao ni
bidii,juhudi,ubunifu na nidhamu.
Wanaoshindana
kwenye kupiga Mbio ni wengi lakini anayechukua tuzo ni mmoja.
JIANDAE
KUSHINDANA NA KUSHINDA.NAKUTAKIA USHINDI KATIKA MWAKA 2015
Post a Comment