Na Ferdinand Shayo,Shayo.
Fursa ni
nafasi ambazo zinaweza kumwingizia kipato mtu na kama zitatumika vizuri na kwa
wakati unaofaa zinaweza kubadilisha
kabisa maisha yako.
Ili kuona
fursa hauhitaji kuwa na mabilioni bali unachohitaji ni kuwa na macho ya kuona
na kutambua fursa ambazo wengine hawazioni.
Katika
mazingira tunayoishi yamejaa fursa
nyingi ambazo zipo hapo hapo ulipo
,wakati unayalaumu mazingira kuna watu wanatajirikia kwenye mazingira hayo hayo
,hapo utagundua kuwa tatizo sio mazingira tatizo ni macho ya kuona fursa.
Macho ya
watu wengi huelekea kwenye vitu vilivyotayari
kwasababu ya uvivu wa kufikiri hawapendi kusumbua akili zao kuvifanya
vile visivyoonekana vionekane kwa maana ya kuvumbua vitu vipya na kubaki kugombania vile vinavyoonekana.
“Mtu mwenye uwezo mzuri wa kuona ni
Yule anayeona vitu ambavyo wengine hawavioni
hata kama wanayo macho ya kuona” kinaeleza kitabu cha cha Maarifa “Chochote kinaweza kuwa kama Dhahabu” kilichoandikwa na Lion Mangole .
Kuna mtu
mmoja aliwahi kusema kuwa “What you see
what you get” akimaanisha kuwa unachokiona ndio unachokipata.
Ukiwauliza
watu wengi wanaona nini katika mazingira yao wanakwambia wanaona
shida,mazingira mabovu ,unakutana na mtu mmoja akimuuliza anakuambia anaona
fursa ya kuanzisha biashara,kampuni,taasisi.
Eneo ni moja
ila macho yanayotazama ni tofauti mmoja anaona fursa wengine wanaona matatizo
ndio maana kuna gepu ya kiuchumi kati ya mtu na mtu ,na gepu hiyo haitakwisha
kama macho yao yataendelea kuona kiutofauti.
Kuwa na
macho yanayoona fursa za kibiashara,kiuchumi ni muhimu kwa kila mtu anayehitaji
fedha hapa duniani.
Ni ukweli
usiopingika kuwa mfumo uliopo hapa duniani ili upate mahitaji muhimu ni lazima
uwe na fedha .
Fedha inapatikana
kwa nguvu ya mbadilishano (power of
exchange) ili upate fedha lazima uwe na kitu cha kubadilishana na fedha aidhaa bidhaa kwa fedha ama huduma kwa fedha.
Mazingira
haya haya tunayoyaona mabovu hayafai
wako wachache wanaoyatumia kuanzisha biashara,taasisi na kufanikiwa ile hali
wengi wakibaki kulalamika.
Mtaalamu
mmoja wa masuala ya uchumi nchini alikua akienda uwanja wa ndege kusafiri
ughaibuni alikutana na vijana kadhaa na wao wakihitaji kuruka na ndege kwenda
nchi za nje alipowauliza maudhui ya safari yao wanakwenda kutafuta maisha kwa
maana ya fursa za kiuchumi ,aliwashangaa kwani wakati huo kuna wageni kutoka
nje wanakimbilia kuja nchini kutumia fursa ambazo wenyeji hawazioni.
Bila kuwa na
macho ya kuona fursa za kiuchumi ni vigumu kufanikiwa ,tatizo sio kuhama sehemu
moja kwenda nyingine kikubwa ni nini unakiona katika mazingira uliyoko.
Unapokuwa na macho ya kuangalia fursa
utagundua kuwa hapo ulipo unatembea kwenye mawe ya dhahabu hivyo huna haja ya kwenda sehemu
nyingine kutafuta dhahabu.
Tusibaki na wimbo
wa kusema kuwa Watanzania ni masikini na kuanza kutafuta nani mchawi
aliyewaloga watanzania .
Kumbe
tatizo ni macho ya watanzania wanatakiwa waamke wafungue macho na akili zao ili
waweze kuona kuona fursa zilizopo kwenye mazingira yao badala ya kuyalalamikia.
“Kufungua macho sio kuamka” Nukuu ya Msanii Fareed Kubanda wa Mwanza .Wako waliofungua
macho wakaziona fursa lakini bado wamelala hawajaamka kwa maana ya kuchukua hatua na kuzitumia
fursa hizo ili ziweze kubadilisha maisha yao.
Fursa za
kibiashara zinaweza kutokana na mahitaji ya watu.Tunapoaangalia mahitaji ya watu
na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini
vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa
ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi chakula,maji,usafiri.
itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka.
0765938008
Post a Comment