PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI ZA HIVI PUNDE, DANNY MRWANDA ASAINI YANGA AWAMWAGA SIMBA USIKU WA KUAMKIA LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
HABARI zilizotufikia usiku huu, zinasema kuwa Mshambuliaji wa timu ya Polisi Moro, Danny Mrwanda, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia...


HABARI zilizotufikia usiku huu, zinasema kuwa Mshambuliaji wa timu ya Polisi Moro, Danny Mrwanda, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, usiku huu.


Imekuwa ni tofauti na mategemeo ya mashabiki walio wengi wa soka kutokana na habari zilizozagaa kuanzia juzi kuwa mchezaji huyo 'eti' alikuwa tayari ameshakamilisha taratibu zote za kujiunga na Klabu ya Simba, ambao walimtaka na kufanya naye mazungumzo.


Kama ambavyo imekuwa kwa timu hizi watani wa jadi kufanyiana 'Kitu Umafia', mara kadhaa kwa kuchukuliana wachezaji na kupandiana dau kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachezaji akiwamo, Mbuyu Twite, na wengineo na ndivyo Yanga walivyofanya tena kwa Mrwanda usiku huu.



Ikumbukwe kuwa Simba, walikuwa wameshatangaza dau la kumsajili mchezaji huyo katika kipindi hichi cha dirisha dogo na tayari taratibu zilikuwa zimekwishaanza.


Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda ili kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa ni majeruhi, na mshambuliaji pekee wa ndani aliyebaki tegemeo akiwa ni Hussein Javu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top