PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BAADA YA KUPIGWA CHINI UWAZIRI: TIBAIJUKA AJIKITA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WAKE
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi mkoani kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani wa...





Wananchi mkoani kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiriki kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.

Wakiongea na ITV wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini hatima ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine waliohusika katika sakata hilo na kumuuondoa waziri Tibaijuka napia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha kumg’oa madarakani kiongozi huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akauti hiyo ya TEGETA ESCROW au la.

Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa kagera Hamimu Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa jana wakati akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam kwa kumuondoa kiongozi huyo huku katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa lini katika akanti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho la kwamba pesa hizo hazirudishi?.

Kwa upande wake aliyekuwa Waziri wa ardhi nyumba na makazi Profesa anna tibaijuka amesema licha Rais kumuondo katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba Pesa hizo alipewa na lugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya TEGETA SCROW ndomaana hakutaka kujiuzulu mapema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top