Moja
kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha likishushwa katika Bandari ya
Dar es Salaam, leo asubuhi. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), leo
limepokea mabehewa 50 ya kubebea makasha ambapo mradi huu unatekelezwa
chini ya Mpango wa Matokeo makubwa sasa(BRN).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk . Shaaban Mwinjaka(mwenye tai ya blue),
akiangalia behewa moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha
yalishuhushuwa katika bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia kwake
ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuniya reli Tanzania(TRL), Mhandisi Amani
Kipalo Kisamfu. Kuwasili kwa mabehewa hayo kutasaidia kupunguza
msongamano wa mizigo ya makasha na kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akifurahia jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Aman
Kipalo Kisamfu, kabla ya kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha katika
bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kulia kwa Mhandisi Kipalo Kisamfu
ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(TPA), Mhandisi Alois Matei.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akisisitiza jambo
wakati wa kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha, leo katika Bandari ya
Dar es Salaam. Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba Menejiment ya
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuyatunza lakini pia na wananchi wanaokaa
pembezoni mwa reli kusaidia Serikali kutunza miundombinu ya reli.(Picha
na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi).
Post a Comment