PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WIKI YA TUMBO JOTO KWA VIONGOZI MJINI DODOMA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
   Dodoma/Dar/Mikoani. Ni wiki ya shida. Wiki hii inatarajiwa kuwa ya vikao mfululizo na mijadala isiyokoma. Ndiyo w...
  

Dodoma/Dar/Mikoani. Ni wiki ya shida. Wiki hii inatarajiwa kuwa ya vikao mfululizo na mijadala isiyokoma. Ndiyo wiki inayotarajiwa kuuweka hadharani mtikisiko wa tano katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wakati ripoti ya uchunguzi wa sakata la IPTL itakapowasilishwa rasmi kwa wabunge na Taifa kwa jumla mjini Dodoma keshokutwa na kuhitimisha minong’ono na uvumi.
Ni wiki ambayo Bunge litaamua juu ya hatua za kuchukua dhidi ya vigogo wa Serikali ambao wamekuwa wakitajwa kuhusika na ufisadi huo wa kuchota au kunufaika na Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Ripoti hiyo inayosubiriwa, itawasilishwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na Zitto Kabwe, ambayo itatoa mapendekezo juu ya hatua za kuchukua.
Wabunge wa vyama mbalimbali, jana walikuwa na vikao kadhaa wakijipanga jinsi ya kushughulikia sakata hilo mara tu ripoti itakapowasilishwa.
Wabunge wa CCM jana jioni walikutana kuwekeana msimamo kuhusu sakata hilo huku kukiwa na taarifa kwamba baadhi yao, hasa walioonyesha kushabikia ripoti hiyo, wamekaripiwa na kupewa mwongozo wa kuilinda Serikali.
Habari za ndani zinasema kuna juhudi kubwa zinafanywa ili kuhakikisha Baraza la Mawaziri halivunjwi kwa mara ya pili, baada ya tukio la mwaka 2007 alipojiuzulu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kutokana na kashfa ya Richmond.
Habari zaidi zilisema, juzi kilifanyika kikao kingine ndani ya Makao Makuu ya CCM, Dodoma kikiwahusisha baadhi ya wabunge, mawaziri na vigogo wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo.
Habari zinasema kikao hicho kilipata muhtasari kutoka ndani ya PAC lakini hakikufikia mwafaka kutokana na baadhi ya wajumbe kupinga kujadili suala hilo mbele ya watuhumiwa na bila kupewa ripoti kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi na Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Vilevile, wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) nao walikutana jana kujipanga kwa ajili ya kushughulikia sakata hilo.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema wameitisha kikao hicho kuwekeana msimamo.
“Tunakwenda kukutana kama Ukawa ili tuwekeane msimamo jinsi gani ya kulishughulikia sakata la ufisadi wa Escrow,” alisema Mnyika.
Ripoti hiyo itawasilishwa huku kukiwa na madai kutoka Ukawa kuwa imevuja na kusambazwa mitaani na baadhi ya kurasa zenye majina ya wahusika zikichomolewa ili kuuhadaa umma.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top